Monday 20 June 2016

EURO 2016: SWITZERLAND YAISHIKA SHATI FRANCE NA KUINGIA 16 BORA


France wameshinda Group A huku Switzerland waliwashika shati France na wao kuingia 16 bora...Kifaa cha France Paul Pogba alicheza vizuri na kugonga mwamba mara 2 kipindi cha kwanza...



Sub Dimitri Payet nae aligonga mwamba baada ya kupokea mpira safi kutoka kwa Moussa Sissoko na kupiga volley hatari...Switzerland nao ilikuwa wapewe penalty wakati Sagna alipomvuta shati Blerim Dzemaili dakika za nyongeza...




France sasa kucheza na mshindi wa 3 kutoka Group C, D au E ndani ya jiji la Lyon Jumapili...



Switzerland watacheza na mshindi wa nafasi ya 2 Group C kwa sasa ni Poland lakini anaweza kuwa Germany au la...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment