Friday 17 June 2016

COPA AMERICA: U.S.A YAILAZA ECUADOR KWA SHIDA


Timu ya taifa ya USA imefanikiwa kuingia nusu fainali ya Copa America kwa kuichapa Ecuador 2-1...Kipindi cha 1 kilikuwa kirahisi sana kwa team USA ambapo Jack Dempsey aliipatia USA bao la mapema mnamo dakika ya 22...USA ilikuwa chini mtu mmoja dakika ya 56, Jermaine Jones, na pia Ecuador walipoteza mtu mmoja, Antonio Valencia, ambao wote walitolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kufanya fujo ...




Ecuador walishambulia sana dakika 45 zilizobaki lakini USA waliweza kuwakabili...USA sasa wanasubiri wacheze na Argetina au Venezuela ambao wanacheza Jumamosi ijayo...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment