Friday 17 June 2016

NBA FINAL 2016: LEBRON JAMES AIPAISHA CAVS NA KULAZIMISHA GAME 7




Cleveland Cavaliers walikuja kucheza si kitoto...Toka mwanzo mpaka mwisho ni vikapu tu kutoka kwa King James na wenzake...Ni timu chache sana ambazo wanaweza kutoka nyuma na kusababisha Game 7...James alimaliza na points zingine 41 pamoja na assists 11 bila kusahau rebounds 8...Curry alikuwa haonekani kabisa na akiingia na kutupa mipira haiingii kabisa...





Golden State walishindwa kufunga baskets nyingi wakati Cavs wao walikuwa wanaingia kwenye rangi (paint) kila drive pamoja na nyingine pembezoni (perimeter)...Stephen Curry hali ilikuwa tete mpaka akapigwa tawi hatari na LeBron  na badae Curry alitolewa nje kwa mara ya kwanza kabisa katika maisha yake ya kikapu akiwa na fouls 6 na kupewa technical foul...


Curry alikasirika sana na kutupa kitu kinacholinda meno na kumgonga shabiki...Ilibidi aombe msamaha na atoke nje kabisa ya uwanja...Bofya hapa upate bahari zaidi.

No comments:

Post a Comment