Thursday 30 June 2016

ARSENAL: THE GUNNERS WAMSAKA KIJANA HATARI KABISA GABRIEL BARBOSA KUTOKA BRAZIL


Arsenal bado wanaendelea kutafuta vifaa hatari kuimarisha safu ya mbele na sasa wameingia Brazil na huko kuna kijana anaitwa Gabriel Barbosa ambae ni hatari kabisa...

Barbosa ni mchezaji ambae anawika huko Brazil akichezea timu ya Santos...Kwenye mtandao hasa FIFA superstars na YouTube huyu dogo anawika sana...


Santos legend Zito ndiye aliyemgundua huyu dogo wakati anacheza futsal dhidi ya Santos akiwa na miaka 8.

Baba yake ambae ni mshabiki sana wa Santos alimpeleka dogo akajaribu timu ya Vila Belmiro.

Huko hakukosea kabisa kwani dogo aliweza kufunga mabao 600 na kutunukiwa jina Gabigol na hiyo ikampatia nafasi katika timu ya vijana ya Brazil.



Dogo anakosa nguvu lakini mpira wake ni wa akili sana na anauwezo wa badilika kutokana na mechi inavyoenda...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment