Wednesday 30 April 2014

NBA: MMILIKI WA LA CLIPPERS AFUNGIWA MAISHA


Donald Sterling amefungiwa maisha na NBA baada ya kujulikana kuwa yeye ni mbaguzi wa rangi...Sterling hatohusika na issue yoyote inayohusu NBA hata kuja kwenye game na mazoezi haruhusiwi na itabidi auze timu yake maana haitajiki tena...Amepigwa faini ya $2.5 milioni ambayo ni faini kubwa kuliko zote NBA...Na hiyo faini itaenda kwenye mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi...

Commissioner wa NBA, Adam Silver, amesema NBA haina nafasi kwa wabaguzi na ameshtushwa sana na huyu mpuuzi tena ni mmiliki wa timu...Magic Johnson amesema Adam Silver ameonyesha uongozi wa hali ya juu....Bofya hapa upate habari zaidi...

CHAMPIONS LEAGUE: REAL MADRID YAIGARAGAZA BAYERN MUNICH


Real Madrid jana usiku iliigaragaza bila huruma Bayern Munich mabao 4 kwa 0...Katika hali ambayo haikutegemewa Real Madrid walikuwa wana kasi sana na uhakika wa pasi zao mpaka zikazaa matunda...Game ilikuwa na vurugu za hapa na pale pia rafu nyingi tu lakini refa ailkuwa makini sana kutuliza mambo...Bao lilipatikana kutoka kichwa kikali kilichopigwa na Sergio Ramos mnamo dakika ya 16 kutokana na set-piece...Huyo huyo Ramos alipachika la pili kutokana na set-piece nyingine iliyopigwa na Di Maria dakika ya 20...Ronaldo nae alionyesha makeke yake pamoja na kupigwa buti mara kadhaa aliipatia timu yake bao baada ya kupokea pasi nzuri ya square kutoka kwa Gareth Bale...Bao hili la Ronaldo limevunja rekodi ya mabao katika kombe la Ulaya la mabao 14 ambayo ilishikiliwa na Lionel Messi, Ruud van Nistaroy na Jose Altafini....


Haikuishia hapo Bayern waliendelea kula kichapo baada ya Ronaldo tena kufunga goli zuri la free-kick baada ya kipiga mpira chini wakati wapinzani wakiruka na hii ilikuwa dakika ya 89...Bayern wamepewa kichapo ambacho hawakutegemea mpaka wakaaza kucheza rafu zisizo na msingi...Sasa Real inasubiri mechi kati ya Chelsea na Atletico Madrid leo usiku...Bofya upate takwimu za mechi...

Tuesday 29 April 2014

EPL: ARSENAL YAINGIA CHAMPIONS LEAGUE KWA MARA YA 17


Arsenal FC jana usiku ilifanikiwa kulinda nafasi yake ya 4 baada ya ushindi mkubwa wa mabao 3-0 Newcastle United...Arsene Wenger alifurahi ukurudi kwa Mesut Ozil na Ramsey maana ndio waliobadilisha game..Hii ni mara ya 17 mfululizo Arsenal inaenda kucheza soka la mabingwa la Ulaya....Bofya hapa upate mambo yalivyo kwenda...

NBA: MMILIKI WA LA CLIPPERS NI MBAGUZI WA RANGI


LA Clippers ni timu kubwa ya NBA na msimu huu imefanya vizuri na kuingia Playoffs lakini pamoja na hayo yote inasemekana mmiliki wake, Donald Sterling, ni mbaguzi wa rangi...Hii imejitokeza hivi juzi tu baada ya kurekodiwa na kimada wake, V. Stiviano, na hizi recordings kuibuka kwenye web site moja machachari sana kwa habari moto moto za watu maarufu TMZ huko Marekani...Kwenye hizo recordings huyo mmiliki anamlalamikia kimada wake kwanini anapiga picha na watu weusi na anaziweka kwenye Instagram na anamwambia asiwalete watu weusi kwenye games za Clippers....

Mmoja wa hao watu ni mchezaji maarufu wa zamani wa LA Lakers Magic Johnson...Wadau wa mchezo huo wakesikitishwa sana na matamshi ya huyo mmiliki na pia wadhamini wa Clippers wameanza kujitoa wakati bosi mkubwa wa NBA, Adam Silver, amesema wanafanya uchunguzi na kwamba uchunguzi utaenda haraka na tutajulishwa hatma ya huyo mmiliki wa Clippers...Max Sports Blog itawaletea habari zaidi kuhusu hii habari siku zijazo... 

PFA: MCHEZAJI BORA WA MWAKA NI LUIS SUAREZ


Luis Suarez amekuwa mchezaji bora wa mwaka...Amepaya tuzo hiyo kutokana na umahiri wake wa kucheza na kufunga magoli mengi...Kwa sasa Suarez anamagoli 30 hapo ukumbuke akikaa bila kucheza mechi 10 baada ya kusimamishwa kwa utovu wa nidhamu baada ya kung'ata Branislav Ivanovic...Baada ya hapo Arsenal walikuwa wanamtaka kwa £40,000 lakini John W. Henry ambaye ni mmiliki wa wa Liverpool aligoma kumuuza...Sasa Suarez ni mchezaji bora wa soka mwaka huu...Hongera zake Suarez kutoka kwa Max Sports Blog...Bofya hapa usome zaidi kuhusu Suarez




Monday 28 April 2014

EPL: GIGGS AIPA MWANGA WA TOCHI MANCHESTER UNITED


Hatimaye Manchester United wameweza kuona mwanga japo ni mwanga wa tochi kutoka kwa mwenzao na mchezaji bora sasa ni kocha Ryan Giggs...Manchester United ilikumbushwa na kocha wao wa muda kwamba Manchester United inaogopwa kwa vitu viwili tu...kasi na kutokata tamaa...na ndivyo walivyo fanya baada ya kuichapa timu hafifu ya Norwich City 4-0...Ushindi huu unakuja baada ya kocha David Moyes kutimuliwa baada ya kuwakosesha nafasi ya kuingia Champions League...

Kuna tetesi ambazo unazipata hapa Max Sports kwa mara ya kwanza kwamba Manchester United iko mbioni kuchukua kocha Louis van Gaal kutoka Uholanzi...Huyu kocha ni kocha ambae hana mzaa na anafundisha national team ya Uholanzi...Amewahi kufundisha timu kubwa kama Ajax, Barcelona, AZ na Bayern Munich...Pia alikuwa midfielder wa timu ya Royal Antwerp, Telstar, Sparta Rotterdam na AZ...Wakiweza kukamilisha mambo na kumchukua huyo Manchester United itarudi top 4...

EPL:BASI LA YUTONG LAIOKOA CHELSEA


Wakati mwingine hatupendi kupanda mabasi lakini ukipanda wakati limepaki ni issue nyingine...Hii imetokea jana kwenye moja ya mechi kubwa sana za ligi ngumu ya Uingereza kati ya Chelsea FC na Liverpool FC katika uwanja wa Anfield....Liverpool ingeshinda ilikuwa inajihakikishia ubingwa lakini Chelsea walikuja kuwazuia...Timu zote zilianza vizuri kwa kujipanga na kufika golini kwa mwenzake lakini baada ya muda kusogea tuliona hali ikibadilika na mashambulizi yakielekezwa kwenye lango la Chelsea...

Chelsea walibadilisha tactics na mid-fielders wote wakarudi nyuma na kupaki basi la Yutong, haya mabasi utakutana nayo ukielekea Mbeya kutoka Dar na pia ukuelekea Kilimanjaro, hii iliwachanganya sana Liverpool maana walikuwa na possession muda mwingi na kila wakijaribu wanagonga tairi mara bodi...Ba wa Chelsea aliiweka Chelsea mbele kwenye dakika ya 45 dakika chache kabla ya muda wa kipindi cha kwanza kuisha baada ya uzembe wa Steve Gerrard...Williams pia aliipachika bao zuri mwishoni kabisa baada ya kupokea mpira kutoka kwa Torres...Bofya hapa upata habari zaidi kuhusu basi la Chelsea...

Saturday 26 April 2014

WORLD SNOOKER CHAMPIONSHIP: O'SULLIVAN AINGIA ROBO FAINALI


Bingwa wa mwaka jana wa Snooker na mmoja wa mabingwa wa mchezo wa Snooker duniani, Ronnie O'Sullivan, ameingia robo fainali baada ya kutoa Joe Perry ambae ni mwingereza mwenzake 13-11.

TENNIS: RAFAEL NADAL AGONGA UKUTA


Rafael Nadal, bingwa wa clay court, amegonga ukuta na kuangukia pua baada ya kuchapwa na Nicolas Armagro huko Barcelona...Nadal amemaliza mechi zake 41 bila kufungwa na sasa ametolewa kwenye robo fainali ya hayo mashindano ya Barcelona...Nadal pia alifungwa kwenye mashindano ya Monte Carlo Masters na David Ferrer...Almargo, namba 20 duniani, ambae amejarubu kumfunga Nadal mara 11 alifanikiwa kumchapa Nadal kwenye match pint ya pili 2-6, 7-6 (5), 6-4...Bofya hapa upate habari zaidi...

LA LIGA: TITO VILANOVA HAS PASSED AWAY

 
Former FC Barcelona coach Tito Vilanova has passed away at age 45.
 

Thursday 24 April 2014

BOXING: MAYWEATHER VS. MAIDANA

Pambano kubwa linakuja May 3 kati ya Floyd Mayweather na Marcos Maidana...Habari zaidi kuhusu pambano hili kali utazipata Max Sports...Hebu cheki tizi kali hapo chini...

NBA PLAYOFFS: BLAZERS WAKO MOTO


Portland Trail Blazers wameshinda Game 2 dakika chache zilizopita...Blazers wamemchapa Houston Rockets 112-105...LaMarcus Adridge afanya mambo na kupachika pointi 43 na hii ni mara ya pili anavuka pointi 40 kwenye game...Hii ni mara ya kwanza mchezaji kupata pointi 40 mara 2 kwenye game toka LeBron James alivyo fanya hivyo Mwezi wa 5, 2009...Dwight Howard nae alikuwa moto kipindi cha kwanza na alipata pointi 25 lakini badae akapunguza kasi...


TANZANIA: BURUNDI YATIA TIMU KESHO KWA MECHI YA KIRAFIKI


Timu ya taifa ya Burundi 'Intamba Mu Rugamba' itakuja kesho nchini kwa mechi ya kimataifa ya kirafiki na Taifa Stars katika uwanja wa Taifa...Afisa wa habari wa TFF (Tanzania Football Federation) bwana Boniface Wambura alisema kwamba timu hiyo ya Burndi itawasili kesho saa 12 jioni wakiingia na Kenya Airways na pia ni katika kusherehekea miaka 50 ya muungano...Bofya upate habari zaidi...

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: REAL MADRID YASHINDA GAME YA KWANZA


Real Madrid ilifanikiwa kushinda game ya kwanza na kuzuia Bayern wasipate goli la ugenini na asante ziende kwa Karim Benzema ambaye alipachika bao dakika ya 19...Bayern walikuwa wameshikilia sana mpira mpaka kuna wakati walifikia asilimia 80 ya possession kipindi cha kwanza...Bayern sasa wana mlima wa kupanda wakirudi nyumbani kwenye ungwe ya pili ya nusu fainali...Real walikosa magoli mazuri akiwemo pia Cristiano Ronaldo...Bofya hapa upate habari zaidi...

Tuesday 22 April 2014

EPL: DAVID MOYEZ ATIMULIWA


Habari tulizozipata muda huu hapa Max Sports ni kwamba Manchester United wamemtimua kocha wao David Moyez...Habari hizi ni njema kwa mashabiki na wadu wa timu ya Manchester United kwani msimu wao umekuwa ovyo mpaka inasemekana wanaongoza kutaniwa...Moyez amekaa kwenye kiti cha ukocha kwa miezi 10 tu...Alifukuzwa leo asubuhi na Ed Woodward ambae ni makamu mwenyekiti wa Mancherster United...Makocha Jimmy Lumsden na Steve Round pia wameondoka na kuacha nafasi zao wazi...Ryan Giggs atachukua uskani na kusimamia timu hiyo kwenye game inayokuja na Norwich City...Bofya hapa upate habari zaidi...

EPL: MATOKEO YA MECHI ZA WEEKEND YA PASAKA

Monday, April 21, 2014
StatusHomeScoreAwayVenue
FT Manchester City 3-1 West Bromwich Albion Etihad Stadium
Saturday, April 19, 2014
StatusHomeScoreAwayVenue
FT Tottenham Hotspur 3-1 Fulham White Hart Lane (35,841)
FT Aston Villa 0-0 Southampton Villa Park (35,134)
FT Cardiff City 1-1 Stoke City Cardiff City Stadium (27,686)
FT Newcastle United 1-2 Swansea City St James' Park (51,057)
FT West Ham United 0-1 Crystal Palace Boleyn Ground (34,977)
FT Chelsea 1-2 Sunderland Stamford Bridge (41,210)

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA


P W D L GD PTS
Liverpool3525555280
Chelsea3523664175
Man City3423565674
Arsenal3521772170
Everton3520962369
Tottenham3519610263
Man Utd34176111657
Southampton35131012549
Newcastle3514417-1546
Stoke35111113-1044
C Palace3513418-1343
West Ham3510718-1037
Swansea359917-436
Hull3410618-936
Aston Villa349817-1435
West Brom3461513-1333
Norwich358819-2832
Cardiff357919-3430
Fulham359323-4230
Sunderland347819-2429

Monday 21 April 2014

BOXING: RUBIN "HURRICANE" CARTER AFARIKI DUNIA


Boxer maarufu katika dunia ya boxing Rubin "Hurricane" Carter amefariki dunia...Alifariki akiwa usingizini huko Toronto Canada kutokana na ugonjwa wa Cancer, Prostate Cancer...Carter ambae alifariki na umri wa miana 76 alikuwa boxer mkali sana miaka ya 60 na alifahamika alivyomtwanga Emile Griffith ambaye alikuwa bingwa 1963 katika round ya kwanza..."Hurrucane" alijaribu 1964 kuchukua ubingwa wa middleweight lakini alichapwa na Joey Giardello...

Rubin "Hurricane" Carter alikuwa tena kwenye habari lakini habari ambazo hazikuwa nzuri ni kwamba alisingiziwa na alipatikana na hatia ya kuua wazungu watatu kweye pub...Alienda jela 1966 mpaka 1985 wakati Jaji mmoja alipomtoa nakusema kesi yake ilikuwa imejaa chuki na ubaguzi wa rangi na hana hatia kabisa...




Toka awe huru alikuwa anapigania haki za wafungwa ambao wameonewa au wamefungwa kwa makosa ambayo sio yao...Denzel Washington mcheza filamu maarufu sana alitengeneza movie kuhusu maisha ya Rubin "Huricane" Carter insyoitwa 'The Hurricane' mwaka 1999...Soma zaidi kuhusu "Hurricane" hapa

EPL: LIVERPOOL YAKARIBIA UBINGWA


Liverpool jana ilikaribia ubingwa baada ya kuichapa Norwich 2-3...Sasa Liverpool wako pointi 5 mbele na wameshindilia nafasi yao ya Champions League msimu ujao...Liverpool hawakupata unafuu kwani walikuwa wanaongoza 2-0 na Norwich wakacheza mpira safi na kuanza kurudisha magoli...Snodgrass aliweza kuingiza goli la kichwa na dakika kama 13 za mwisho zilikuwa mshike mshike wakati Norwich wakijaribu kubadilisha matokeo...Liverpool ikishinda Premiership itakuwa mara yao ya kwanza toka Premiership ianzishwe...Bofya upate habari zaidi...

NBA PLAYOFFS: BLAZERS YASHINDA GAME 1

LaMarcus Aldridge 

Portland Trail Blazers iliweza kushinda game ngumu na kali dhidi ya Houston Rockets 122-120...Game ilikuwa kali sana mpaka mwisho maana timu zote zilikuwa moto balaa...Jina ambalo lilisikika sana usiku wa game ni LaMarcus Aldridge ambaye alikuwa anarusha na kuingiza tu...LaMarcus aliweka rekodi ya points ambapo alipata points 46...Points hizo ni mara ya kwanza yeye kama yeye ameweza kupata pia ni rekodi ya timu yake kipindi cha playoffs...Houston wangeweza sawazisha lakini Harden aligonga mwamba kabla kengele ya kumaliza game...Paya habari zaidi za hii game hapa...


F1: LEWIS HAMILTON ASHINDA TENA


Lewis Hamilton ametimiza ndoto yake ya kushinda mashindano ya Formula One mara tatu mfululizo na timu ya Mercedes...Hamilton alishinda Grand Prix ya China kwa kuwa makini toka mwanzo wa mashindano na kuongoza mpaka mwisho...Mercedes walipata ushindi huo ambao ulijumuisha nafasi mbili za kwanza...Aliyechukua afasi ya 3 ni Alonzo kutoka timu ya Ferrari...Mashindano haya ya China yalikuwa na ushindani mkubwa hasa kupigania nafasi ya 2 na ya 3...Sasa Mercedes wanaongoza kwenye kundi la timu za F1...Bofya hapa upate habari zaidi...

Sunday 20 April 2014

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA


CLUBPWDLGDPTS
Liverpool3424555177
Chelsea3523664175
Man City3322565471
Arsenal3420771867
Everton3419962166
Tottenham3519610263
Man Utd33176101857
Southampton35131012549
Newcastle3514417-1546
Stoke35111113-1044
C Palace3513418-1343
West Ham3510718-1037
Swansea359917-436
Hull3310617-636
Aston Villa349817-1435
West Brom3361512-1133
Norwich348818-2732
Cardiff357919-3430
Fulham359323-4230
Sunderland347819-2429