Thursday 31 July 2014

SQUASH: Case Swedish Open 2014 - Final Roundup Ashour v Matthew

SQUASH: Swedish Open in Squash 2014 - Final

EPL: SPRAY YA WORLD CUP KUTUMIKA PREMIERSHIP



Spray maarufu ambayo ilitumika kwenye World Cup ya mwaka huu huko Brazil kwaajili ya kudhibiti washezaji wasisogee wakati set-piece hasa free-kick itatumika kwenye Premiership msimu ujao...Hii spray ambayo anatembea nayo refa huyeyuka baada ya kutumika...


Boss wa Premiership Richard Scudamore amesema baada ya kuona mafanikio ya kutumia hiyo spray na baada ya kuongea na timu na wadau wa premiership sasa hiyo spray itatumika kwenye msimu ujao...Pia amesema premiership iko tayari kubadilika kama mabadiliko yataisaidia mchezo wa soka...Bofya hapa upate habari zaidi...

CHAMPIONS LEAGUE: CELTIC YAGARAGAZWA NA LEGIA


Celtic imegaragazwa vibaya na Legia Warsaw kwenye mechi ya round ya 3 ya kufuzu kucheza Champions League...Isingekuwa kipa Fraser Forster mabao yangekuwa mengi sana...Efe Ambrose alipewa kadi nyekundu baada ya rafu mbaya...Celtic walianza kuona lango la Warsaw lakini walijichanganya na wakalamba 2 kabla ya mapumziko...Game ilimalizika kwa mabao 4-1...Bofya hapa upate habari zaidi...

Wednesday 30 July 2014

EPL: LUKAKU MBIONI KUBAKI EVERTON


Romelu Lukaku yuko mbioni kuhamia Everton moja kwa moja kwa mkataba wa miaka 5...Habari ambazo ni zakuaminika zimesema Lukaku atachukuliwa kwa kiasi kikubwa...Lukaku ambae anamiaka 21 alikuwa Everton kwa mkopo kutoka Chelsea na toka aingie Everton amefunga mabao 16 msimu uliopita na kuisaidia Everton kuingia Europe baada yamiaka 5...Chelsea ilimnunua Lukaku kutok Anderlecht kwa milioni 18... 

Tuesday 29 July 2014

FRENCH LEAGUE 1: AYEW AENDA LORIENT


Jordan Ayew Ghanaian International ametia saini mkataba na timu ya League 1 ya Lorient...

GLASGOW 2014: OKAGBARE ASHINDA MBIO ZA MITA 100


Blessing Okagbare kutoka Nigeria ameshinda mbio maarufu za mita 100...Okagbare alitumia muda wa sekunde 10.85...Aliwashinda wenzake kutoka Jamaica Veronica Campbell-Bown na Kerron Stewart ambao walipata Silver na Bronze wa 4 alikuwa Asha Philip kutoka Uingereza...Okagbare ambae anamiaka 25 atakimbia mita 200 na long jump pia...Mpaka sasa Nigeria wana 10 medals...

GLASGOW 2014: BINGWA WA SQUASH DUNIANI ASHINDA DHAHABU


Bingwa wa Squash duniani na namba 1 duniani kwa upande wa wanawake ameshinda mashindano ya Squash kwenye michezo ya Commonwealth huko Glasgow Scotland...


Nicol David  alimchapa Laura Massaro 12-10, 11-2, 11-5...Nicol ni bingwa wa dunia kwa miezi 99 sasa na hii ni mara ya pili anashinda dhahabu kwenye michezo ya Commonwealth...Bofya hapa upate habari zaidi...

Monday 28 July 2014

EPL: ARSENAL YASEMA OSPINA TAYARI


Arsenal FC imekamilisha usajili wa David Ospina kipa mkali sana kutoka Nice...Ospina ambae nchi yake ni Colombia atakaa Emirates miaka 4 na amechukuliwa kwa milioni 3.2 pounds...Ospina mwenye umri wa miaka 25 atakuwa karibu na kipa namba 1 wa Arsenal Sczcesny na itabidi apambane na yeye awe namba 1...Huyu ni mchezaji wa 3 kuingia Emirates mwaka huu...Arsenal nao wameamua kuchukua vifaa vya nguvu maana huwa ni wazito kutumia pesa nyingi kununua vifaa...Bofya hapa usome zaidi....

YANGA: KAMATI KUU YAVUNJWA NA KUUNDWA UPYA

Manji na Sanga (picha: michuzi blog)
Taarifa zilizotoka Jangwani kupitia Secretary General wa club ya bwana Beno Njovu kwa waandishi wa habari zimesema kwamba kwa mujibu wa katiba ya club mwekiti Yusuf Manji na makamu mwenyekiti Clement Sanga wana wajibu wa kubadilisha kamati ilikukabiliana na mabadiliko katika club hiyo kongwe...Clement Sanga amewataja wanakamati wapya ambao ni Abbas Tarimba, George Fumbuka, Waziri Barnabas, Sam Mapande na Abubakar Rajab...Wengine ni Mohamed Nyange, Musa Katabalo, Seif Ahmed, David Sokoine, Isaac Chanji na Mohamed Bhinda...Sanga amesema hawa wote watasimamia kamati za nidhamu, uchaguzi, technical, uchumi na ushindani....Pia amesema watingia kombe la Kagame....Bofya hapa upate habari zaidi...

TANZANIA U-17: RC AFUNGUA MASHINDANO YA VIJANA


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiq amefungua mashindano ya vijana ya kikanda yanayoitwa 'Airtel Rising Stars'...Sadiki amewaasa TFF na wadau wa mpira kuchukulia kwa uzito umuhimu wa kuwafundisha vijana michezo toka wadogo...Aliwakumbusha wadau kwamba michezo ni muhimu sana katika maendeleo yao ya elimu na pia katika kutafuta ajira au kujiajiri...Bofya hapa usome zaidi...

Sunday 27 July 2014

BOXING: ROY JONES JR. AMTWANGA FRY


Roy Jones Jr. ameshinda pambano lake dhidi ya Courtney Fry huko Riga Latvia...Jones Jr. limtwanga Fry na kushinda kwa TKO baada ya Fry kishindwa kuendelea kutokana na kuchanika karibu na jicho...Pambano lilikuwa chini ya uzito wa cruiserweight...Jones ambae umri umeenda sasa anatakiwa kustaafu lakini ubishi wake umempa ushindi na kufikisha 58-8 (41KO's)...Jones anamkono mwepesi na alifnikiwa kupeleka Fry chini round ya 5 baada ya kurusha uppercut kali iliyomkuta na kumpa kizunguzungu Fry...Bofya hapa upate habari zaidi...

Saturday 26 July 2014

GLASGOW 2014: BOLT ATAKIMBIA 4X100M


Husein Bolt bingwa washiriki mbio za riadha duniani amesema atashiriki mbio za 4x100m...Hii ni mara ya kwanza Bolt anashiriki michezo ya Commonwealth...Hii ni habari njema kwa wadau wa michezo kwani Bolt ni bingwa wa Olympic mara 6 na ataongeza hamasa kwa watazamaji na waandaaji wa michezo ya Commonwealth...Bolt alipotea kwa muda kutokana na kuumia mguu na sasa yuko fit kuwakilisha nchi yake ya Jamaica...Bofya hapa upate habari zaidi...

EPL: ARSENAL KUMYAKUA BEKI CALUM CHAMBERS


Arsenal FC karibu inamchukua beki makini kutoka Southampton Calum Chambers...Chambers ambae anaichezea Uingereza kwenye timu ya vijana chini ya miaka 19 alichekiwa na madaktari Ijumaa tayari kuingia Emirates...Arsenal wametoa milioni 16 pounds kumyakua beki huyu mkali...Chambers sasa ni mchezaji wa 3 kuingia Arsenal kabla msimu haujaanza wengine ni Alexis Sanches na Mathieu Debuchy...Bofya hapa upate habari zaidi...

F1: GARI YA HAMILTON YAWAKA MOTO


Gari ya Lewis Hamilton imewaka moto katika practice ya mwisho kabla ya mashindano ya Hungary GP kesho...Nico Rosberg ataanza kwenye pole na hii sio habari njema kwa Lewis kwani anapoteza points ambazo zingemwezesha kuwa bingwa...Hii ni mara ya 6 sasa Lewis anapata matatizo kwenye qualifying na kukosa nafasi ya kwanza...Mercedes wanasema wanadhani Hamilton alipata tatizo la kuvuja kwa mafuta...Bofya hapa upate habari zaidi...


EPL: DROGBA ARUDI CHELSEA


Didier Drogba amerudi tena Stamford Bridge....Drogba ambae baada ya kutoka Galatasaray aliamua kuwa free agent sasa ataicheze timu yake ya zamani kwa transfer ambayo ilikuwa free...Jose kocha wa Chelsea amesema Drogba anakuja Chelsea kwasababu ni striker mkali sana Ulaya...Drogba aliichezea Chelsea mara 341 na kufung mabao 157...Bofya hapa upate habari zaidi...

Friday 25 July 2014

GLASGOW 2014: TANZANIA YAANZA VIZURI KWENYE SWIMMING


Tanzania imeanza vizuri kwenye mashindano ya kuogelea...Ammaar Ghadiyali alikuwa kinara wa kuogelea baada ya kushinda mzunguko wa kwanza wa mita 50 za Butterfly...Alitumia sekunde 28.11 na kuwaacha mbali wapinzani wake kutoka St. Vincent na Granadines...Usisahau kuangalia mashindano haya yanayoendelea huko Glasgow Scotland...Bofya hapa upate habari zaidi...

GLASGOW 2014: UFUNGUZI WA MICHEZO YA COMMONWEALTH


Kama ulikosa kuangaliaa ufunguzi wa michezo ya Commonwealth huko Glasgow Scotland sasa unaweza kuangalia ufunguzi huo hapo juu...Malkia wa Uingereza ndie aliyefungua hayo mashindano rasmi...Enjoy...

Thursday 24 July 2014

F1: MEXICO GP YARUDI TENA TOKA 1992

Nigel Mansell (katikati) akishanglilia ushindi 1992 Mexico...
Kushoto ni Riccardo Patrese na kulia ni Michael Schumacher
Grand Prix ya Mexico yarudi tena 2015 baada yakupotea miaka mingi sana...Boss wa F1 Bernie Ecclestone amethibitisha hii na kusema itasaidia pande zote mbili kwa miaka mingi...Miaka 23 sasa toka mashindano ya mwisho kwenye track ya Autodromo Hermanos Rodriguez...Track hiyo ilikuwa inatumika toka mwaka 1963-1970 na 1986-1992...Mtu wa mwisho kushind Mexican GP alikuwa Nigel Mansell kutoka Uingereza akiwa na timu ya Williams-Renault...

Washindi wa Mexican Grand Prix  

Year
Driver
Team
1992
Nigel Mansell (GB)
Williams-Renault
1991
Riccardo Patrese (Ita)
Williams-Renault
1990
Alain Prost (Fra)
Ferrari
1989
Ayrton Senna (Bra)
McLaren-Honda
1988
Alain Prost (Fra)
McLaren-Honda
1987
Nigel Mansell (GB)
Williams-Honda
1986
Gerhard Berger (Aust)
Benetton-BMW
Pia boss wa F1 anasema wako kwenye mazungumzo na Azerbaijan ili waweze pia kutayarisha mashindano ya F1...Azerbaijan wenye utajiri wa mafuta wanataka kutayarisha mashindano ambayo yatapita mitaa ya kawaida mjini Baku...Bofya hapa upate hari zaidi....

GLASGOW 2014: MICHEZO YA COMMONWEALTH YAANZA RASMI


Michezo ya Commonwealth imeanza rasmi huko Glasgow Scotland...Michezo hii inahusisha nchi 71 ambazo zilitawaliwa na Uingereza miaka ya nyuma...Tanzania tulijiunga na Commonwealth mwaka 1961 na mwaka 1962 tulianza kushiriki michezo ya Commonwealth..1974 ndio mara ya kwanza Tanzania inapata medani ya dhahabu ambayo Filbert Bayi ndio alioipata huko Christchurch New Zealand...


Malkia wa Uingereza alifungua michezo hii rasmi mbela ya watu 40,000 waliokuwa uwanja wa Celtic Park na mamilioni waliangalia ufunguzi huo kwenye tv..Bofya hapa upate habari zaidi...

ELP: MANCHESTER UNITED YAANZA VIZURI CHINI YA KOCHA MPYA

Ander Herrera 
Manchester United imeanza vizuri chini ya kocha wao mpya Van Gaal baada ya kuigaragaza LA Galaxy 7-0...LA Galaxy walikula kichapo mbele ya watu 86,432 Rose Bowl California...Dakika ya 13 tu Danny Welbeck alifungulia magoli...Hii ni mchi ya kwanza kati ya mechi 4 za ziara ya Man U nchini Marekani...Timu ilikuwa chini ya captain Darren Fletcher...Wengine waliofunga ni Ashley Young mabao 2 na beki Reece James mabao 2...Dogo Ander Herrera alioingia Man U juzi tu alikuwa kwenye 1st 11...Bofya hapa usome zaidi...

Wednesday 23 July 2014

FURSA: WADAU WA MAX SPORTS CHANGAMKIENI FURSA NYINGINE


Wadau wa Max Sports kuna fursa hapa ya kuanzisha garage na car wash kwa wale wanaopenda biashara hiyo...Hebu soma hiyo picha hapo juu na upate maelezo ya vitu ambavyo ni vipya kabisa na vinapatikana hapa Dar es salaam...Piga simu iliyo hapo juu kwa maelezo zaidi...

Tuesday 22 July 2014

BRAZIL: DUNGA KOCHA TENA


Carlos Dunga amechaguliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil...Hii ni mara ya 2 Dunga anaifundisha timu ya Brazil mara ya kwanza ilikuwa 2006 mpaka 2011...Dunga pia aliwahi kuichezea timu ya ushindi ya Brazil mwaka 1994 wakati akiwa captain...Dunga anachukua nafasi ya Luiz Filipe Scolari ambae aliamua kustaafu baada ya kukosa kombe la dunia...Bofya hapa upate habari zaidi...

LA LIGA: REAL MADRID YAMNYAKUA MSHINDI WA GOLDEN BOOT


Real Madrid imechukua kifaa cha ukweli na mshindi wa Golden Boot kwenye World Cup iliyopita James Rodriguez...Forward huyu mwenye miaka 23 kutoka Colombia amechukuliwa kwa pound milioni 63...Hii transfer sasa ni ya 4 kwa pesa nyingi iliyotumika kumyakua mchezaji...Transfer ya bei mbaya ni ile ya Gareth Bale na kufuatiwa na Cristiano Ronaldo na Luis Suarez...Bofya hapa upate habari zaidi...

EPL: PATRICE EVRA AHAMIA JUVENTUS


Partice Evra amekamilish uhamisho wake kutoka Man U kwenda Juventus...Evra amechukuliwa wa pound milioni 1.2...Evra aliingia Man u kutokea Monako kwa pound milioni 5.5 miaka 8 iliyopita na ameshinda Premiership mara 5 akiwa na Man U...


Evra aondoka Man U akimshukuru sana Sir. Alex Ferguson kwa kumwezesha awe captain na kumkumbusha hakuna aliye juu ya club...Bofya hapa upate habari zaidi....

EPL: STEVE GERRARD ASTAAAFU SOKA LA KIMATAIFA


Steve Gerrard ameamua kustaafu soka la kimataifa baada ya kutumikia nchi yake kwa miaka 14...Gerrard ambae alianza kuitumikia nchi yake mwaka 2000 chini ya kocha makini Kevin Keegan katika ubingwa wa Ulaya...Gerrard ana 114 caps (mechi 114 za kimataifa alizoichezea nchi yake) na game yake ya mwisho ilikuwa dhidi ya Costa Rica...

Kijana Steve akiwa na Kevin Keegan akiwa 

Gerrard amecheza kwenye timu ya taifa ya Uingereza chini ya makocha 6 ambao ni Kevin Keegan, Peter Taylor, Sven Goran-Eriksson, Steve McClaren, Fabio Capello na Roy Hodgson...Katika muda huo amefunga mabao 14...Goli lake la kwanza la kimataifa lilikuwa mwaka 2001 walipoichapa Ujerumani 5-1 huko Munich...Bofya hapa upate habari zaidi...

Monday 21 July 2014

EPL: LIVERPOOL IKO MBIONI KUMYAKUA LOIC REMY


Liverpool sasa inahakikisha kikosi chake kiko imara kwa kumtaka mfaransa Loic Remy kutoka QPR...Remy alikuwa Newcastle kwa mkopo baada ya QPR kuwa relegated na pia alikuwa kwenye squad ya timu ya taifa ya Ufaransa iliyofika robo fainali kwenye World Cup huko Brazil...Huyu dogo alimaliza ligi na magoli 14...Huu ni wakati mzuri hasa kwakuwa Liverpool ilimwachia Fabio Borini aondoke kwa pound milioni 14 hivi majuzi tu...Remy atachukuliwa na timu hiyo ya Merseyside huko kaskazini magharibi kwa pound milioni 8.5...Bofya hapa upate habari zaidi... 

AFCON 2015: TAIFA STARS YATOKA SARE NA MAMBAS

Mchezaji wa Stars akimtoka mtu...(Picha kutoka Shaffidauda.com)

Taifa Stars jana jioni ilishindwa kushikilia ushindi baada ya mchezo kumalizika 2-2...Khamis Mcha ambaye alikuwa substitute ndio aliyekuwa kinara wa magoli...Nooij kocha wa Taifa Stars alisaidia kutoa siri ya Mambas jinsi gani ya kuwakabili na ikasaidia...Mambas hawajawahi kupoteza mechi dhidi ya Stars...Tusubiri marudiano huko kwao sasa...Sehemu nyingine Uganda imeshinda mechi yake dhidi ya Mauritania 2-0 huko Kampala Uganda...Bao la kwanza ililikuja kipindi cha 2 dakika ya 49 baada ya Brian Majwega kunyuka mkwaju safi...Bofya hapa upate habari zaidi...

Sunday 20 July 2014

THE OPEN CHAMPIONSHIP: RORY MCLLROY BINGWA


Rory Mcllroy ashinda British Open leo baada ya kufukuziwa na Sergio Garcia na Rickie Fowler...Rory alishinda kwa stroke 2 na alipata 71 na ameondoka na kitita cha dola za kimarekani milioni 8...Dogo kutoka Ireland ya kaskazini ameshinda Major ya 3 sasa akiwa na miaka 25 tu...Rory sasa ni namba 2 duniani kwenye rankings za golf...Bofya hapa upate habari zaidi...

F1: HAMILTON AIBUKA MSHINDI WA 3 WAKATI ALIANZA WA 20


Nico Rosberg amenyakua German GP...Gumzo nililikuwa kwa Hamilton leo jinsi alivyoonyesha umahiri wake wa kuendesha baada ya kuanza wa 20 kwenye grid na kumalizia wa 3...


Hamilton alianza wa 20 kutokana na ajali mbaya aliyoipata jana baada ya gari yake kupata matatizo ya breaks...Mshindi wa 2 alikuwa Bottas na mshindi wa 4 Sebastian Vettel...Bofya hapa upate habari zaidi...

AFCON 2015: TAIFA STARS UWANJANI LEO NA MAMBAS


Taifa Stars watinga uwanjani leo kwenye uwanja wa taifa kupambana na 'Mambas' kutoka Mozambique...Hii ni mechi muhimu sana ya round ya pili katika kampeni ya kuelekea AFCON 2015...Kocha wa Taifa Stars Mart Nooij anakutana na timu yake ya zamani leo...Nooij aliwafundisha Mambas kati ya mwaka 2007 na 2011...Hii ni mara ya 5 timu hizi zinakutana kwenye michuano ya AFCON...Max Sports inawatakia heri Taifa Stars kwenye mechi yao ya leo...Bofya hapa usome zaidi...

Saturday 19 July 2014

EPL: ROBBIE FOWLER ATEULIWA BALOZI WA LIVERPOOL


Robbie Fowler amerudi tena Liverpool kama Balozi...Striker hatari sana ambae alianzia maisha yake ya soka hapo Liverpool academy na kungia timu ya wakubwa 1993...Amecheza mechi 369 na kati ya hizo alipata mabao 183...Robbie amesema ilikuwa heshima kuichezea Liverpool na miaka 30 hapo Liverpoool imekuwa ni kipande cha maisha yake...Kwa wale wadau wa Merseyside anamuita Fowler "Legend" kwani huyu striker alikuwa mkali sana na anakasi kubwa sana...Hapo chini angalia jinsi alivyokuwa anacheza enzi zake...Hongera sana Balozi Robbie Fowler...


Friday 18 July 2014

LA LIGA: TONI KROSS SASA NI MCHEZAJI RASMI WA REAL MADRID

Toni akiwafurahisha mashabiki wa Madrid

Toni Kross amekamilisha usajili wake Real Madrid kutoka Bayern Munich...Kross amechukuliwa na Real Madrid kwa milioni 24 pound za Uingereza...


Toni na Ancelotti

Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amemshukuru Kross kwa muda wake Bayern na anamtakia heri yeye na familia yake huko Madrid...Bofya hapa upate habari zaidi...

EPL: VAN GAAL ASEMA SURA MPYA ZITAKUJA


Kocha mpya wa Manchester United mesema inawezekana sura mpya zikajitokeza lakini hii ni baada ya yeyey kocha kuwaangalia wachezaji aliokuwanao kwanza...Atachukua wiki 3 au 4 kuangalia squad yake itavyojituma chini yake alafu ataamua kama aongeze wachezaji au la...Van Gaal pia amesema ataangalia jinsi ya kuwatumia vizuri Rayan Giggs, Nicky Butt, Phil Neville na Paul Scholes kwenye mambo yake ya ukocha...Angalia hapo chini press conference yake ya kwanza toka ajiunge na club hiyo...


BOXING: PAC-MAN KUZICHAPA NA CHRIS ALGIERI


Pac-Man

Manny 'Pac-Man' Pacquiao atarudi tena ulingoni kuzichapa na Chris Algieri (20-0, 8 KO's)November 22 huko Macao China...Chris Algieri hafahamiki sana lakini ni boxer mzuri sana na pia ni bingwa WBO junior welterweight kwahiyo Pac-Man atakuwa na mtihani mkubwa... 

Chris Algieri

Mkanda utaokuwa unatafutwa na Chris Algieri ni wa WBO welterweight ambao umeshikiliwa na Pac-Man...Algieri alipanda ngazi baada ya kuntwanga Provodnikov hivi karibuni...Hii ni mara ya 2 Pac-Man anazichapa huko Macau...Mwaka jana alizichapa na Brandon Rios hatika huo mji unaojulikana sana duniani kwa kamali...Usikose kuangalia...

Thursday 17 July 2014

EPL: ARSENAL YAIMARISHA KIKOSI TENA KWA KUMCHUKUA DEBUCHY


Mathieu Debuchy sasa ni mchezaji rasmi wa Arsenal FC...The Gunners wameongeza kifaa hichi kipya ili kuimarisha kikosi chake na pia ni baada ya kumnyakua Alexis Sanchez...Debuchy ni full-back hatari sana kutoka Newcastle na pia yuko katika timu ya tifa ya Ufaransa amechukuliwa kwa kiwango ambacho hakijatajwa bado lakini wadu wanasema inawezekana ni milioni 12 pouns za Uingereza...Arsene Wenger amesema Arsenal inafuraha ya kumkaribisha Debuchy Arsenal FC...Bofya hapa upate habari zaidi....

Wednesday 16 July 2014

GLASGOW COMMONWEALTH GAMES: DR. KIKWETE AWATAKIA HERI WANARIADHA

Rais Dr. Kikwete akimkabidhi nahodha wa timu ya riadha (picha: www.ikulu,go.tz)

Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amewatakia heri timu ambayo itatuwakilisha kwenye michezo Commonwealth huko Glasgow...Rais Kikwete amewaambia wanariadha 39 amabo watatuwakilisha kwamba wanadeni na kulilipa hilo deni ni kurudi na ushindi...Amesema pia Tanzania kuna ukame wa medals na sasa ni wakati wa kubadilisha mambo...Rais amewashukuru Tanzania Olympic Committee pamoja Wizara ya Vijana na Wizara ya Mambo ya Nje kwa kuhakikisha timu iko katika hali ya kimataifa na iko tayari kupambana katika hiyo michezo ya Commonwealth...Bofya hapa upate habari zaidi...

EPL: ARSENAL WAKO TAYARI KUTOA MAMILIONI KUMCHUKUA KHEDIRA


Arsenal FC iko tayari kutoa milioni 20 pound za Uingereza kunyakua midfielder hatari sana kutoka Real Madrid Sami Khedira...Inasemakana Khedira atakubali mkataba wa miaka 4 na Arsenal...Arsene Wenger atakuwa ameimarisha kikosi kwa kusajili watu 2 sasa baada ya kumchukua Alexis Sanchez...Mjerumani Khedira inasemekana ameboreka na Real Madrid na amegoma kusaini mkataba mpya na timu hiyo...Bofya hapa upate habari zaidi...

Tuesday 15 July 2014

CHESS: TANZANIA KWA MARA YA KWANZA YAPATA FIDE RANKINGS


Kwa mara ya kwanza katika historia Tanzania imepata FIDE (Shirikisho la Chess Duniani) rankings...Wachezaji 5 kutoka Tanzania wamepata ranking hizo za FIDE...Mwenyekiti wa Tanzania Chess Association, Geoffrey Mwanyika, alithibitisha haya na kuwataja waliopata rankings hizo ni pamoja na yeye Mwenyekiti (1922) Hemed Mlawa (1799) Yusuf Mdoe (1707) Mwaisumbe Emmanuel (1685) na Godlove Kimaro (1681)...


Georfrey Mwanyika (kushoto) akiwa na bingwa wa dunia Vishy Anand (katikati)

Mwanyika amesema sasa hawa wote wananafasi ya kuwa International Master na Grand Master...Sasa Tanzania kwa mara ya kwanza iko mbioni kutafuta Grand Master wa kwanza...FIDE walitangaza hizi ranking mpya baada ya michuano iliyofanyika hivi karibuni kati ya Kenya na Tanzania iliyoandaliwa na Spicenet na Kasparov Chess Foundation...Safi sana wachezaji wote wenye hizo ranking za kimataifa na Max Sports pamoja na wadau tunawatakia heri katika kutafuta Grand Master wa kwanza wa Tanzania...

EPL: LIVERPOOL SANA YAMTAKA MARCO REUS


Liverpool FC au wazee wa Anfield wanamtaka sana dogo kutoka Borussia Dortmund Marco Reus....Reus alitoswa na Barca wakati Suarez alipochaguliwa na Barc...Liverpool wanahitaji sana striker mkali baada ya kumpoteza Suarez...Rogers yuko tayari kutoa milioni 44 pound za Uingereza amchukue Reus...Pata habari zaidi hapa....

AFRICAN YOUTH CHAMPIONSHIP: TIMU YA TAIFA YA VIJANA WAKO TAYARI KUWAKABILI AMABIMBOS


Serengeti Boys timu yetu ya taifa ya vijana (U-17) ijumaa itaingia uwanjani na vijana wenzao kutoka Afrika ya Kusini...Timu hiyo inayojulikana kama Amajimbos watachuana na Serengeti Boys kwenye mashindano ya awali wa African Youth Championship katika uwanja wa Azam Complex huko Chamanzi Dar es Salaam...Kocha mpya wa Serengeti Boys amesema wamewaweka vijana wake tayari kwa mechi ya ijumaa wakijua kwamba madogo wa Amajimbos wanacheza kwa misuli na kwamba itakuwa mechi ya kutumia nguvu zaidi...Bofya hapa usome zaidi...

WORLD CUP 2014: KIGEZO CHA MESSI KUSHINDA GOLDEN BALL


Lionel Messi andie aliyeshinda Golden Ball kwenye World Cup iliyomalizika hivi majuzi tu...Sasa wadau wengi hawakutegemea kama Messi angeshinda tuzo hiyo ya mchezaji bora duniani...Hata Sepp Blatter rais wa shirikisho la soka duniani FIFA ameshangaa Messi kushinda tuzo hiyo pia Dieg Maradona nae ameshangaa Messi kuewa tuzo hiyo Maradona anasema James Rodriguez wa Colombia alicheza vizuri zaidi...Ndio imeshangaza wengi lakini takwimu zinasema tofauti...Hebu tafakari hizo takwimu hapo juu ujionee mwenyewe...

EPL: MANCHESTER UNITED SIGNED A BILLION $ DEAL WITH ADIDAS




Adidas has dished out $1.3 billion to Manchester United for making jerseys for the 2015-16 season.

Monday 14 July 2014

WORLD CUP 2014: LUIZ FILIPE SCOLARI ABWAGA MANYANGA


Kocha maarufu sana wa Brazil Luiz Filipe Scolari ameamua kuachi ngazi baada ya kushindwa kunyakua kombe la dunia mwaka huu...Scolari ndio aliowezesha timu ya 2002 kunyakua ubingwa wa dunia lakini kipindi hiki alichemsha...Wengi walimlaumu kocha huyo kwa kutofanya vizuri na kutokuwa na kikosi imara...Brazil walitandikwa 7-1 na Ujerumani na wakachapwa 3-0 na Netherlands...Siku hiyo walipochapwa na Netherlands kila picha ya Scolari ikitokea kwenye tv alizomewa...Lakini pamoja na kutofanya vizuri kipindi hiki Scolari ni kocha mzuri na anaheshimika duniani...Bofya hapa usome zaidi...