Wednesday 2 July 2014

WORLD CUP 2014: USA YARUDISHWA NYUMBANI NA BELGIUM




USA wamefunga virago na kuelekea nyumbani baada ya kuchapwa 2-1 na Belgium kwenye uwanja wa Arena Fonte Nova.


USA walijitahidi sana lakini mwishoni Belgium walikomaa na kulinda lango lao.

Kinara wa mchezo alikuwa kipa mahiri sana wa USA Tim Howard.

Tim ameweka rekodi ya World Cup ya kuokoa mashuti mengi (15) kuliko makipa wote.

Tim aliokoa mashuti makali mengi kutoka kwa Belgium na kuisaidia USA ibakie na moyo wa kushinda.



Game iliingia dakika za nyongeza baada ya kutoka sare.

Belgium ndio walikuwa wa kwanza liona lango la USA baada ya De Bruyne kuwazunguka mabeki na kupachika bao kwenye dakika ya 93.

Romelu Lukaku nae dakika ya 105 aliandika bao la 2.

USA hawakukata tamaa na kwenye dakika ya 107 Julian Green alipachika bao zuri sana ambalo wadau wa tennis wanaita 'volley'.

Green aligusa mpira kwa mara ya kwanza na likawa bao..Bofya hapa upate habari zaidi...

No comments:

Post a Comment