Wednesday 2 July 2014

WIMBLEDON 2014: NADAL APELEKWA SHULE NA DOGO KYRGOIS

Kyrgios akishangalia ushindi wake
 Rafa Nadal alipelekwa shule na dogo ambaye hajulikani sana katika ulimwengu wa tennis...Dogo Nick Kyrgios anatokea Australia ana miaka 19 na ni namba 144 duniani alimfunga bingwa wa dunia na namba 1 duniani Rafael Nadal 7-6 (7-5) 5-7 7-6 (7-5) 6-3...Kyrgios ni mara ya kwanza kucheza center court alionyesha umahiri wake wa kucheza hasa wakati wa kuserve...
 
Dogo alichapa Ace hapa

Kyrgios alimchapa Nadal na 37 Aces wakati Nadal alipata 11 tu...Huyu dogo ni balaa na akiendelea hivi atakuwa mkali sana miaka inayokuja hata Andy Murry na Pat Cash wanafikiria huyu dogo atakuwa mkali sana mbeleni...

Mashabiki wa Autralia wakishangilia kwa furaha
Toka 1992 hakuna bingwa aliyetolewa kwenye Grand Slam na mtu ambaye ana ranking chini...Bofya hapa upate habari zaidi...


No comments:

Post a Comment