Sunday 28 June 2015

BOCA JUNIORS: TEVES AKAMILISHA USAJILI BOCA


Carlos Tevez amerejea tena Boca Juniors alipoanzia mpira wake kabla ya kwenda kucheza Ulaya...Juventus tayari wameshapata mchezaji mbadala ambae ni Mario Mandzukic kutoka Atletico...Bofya hapa upate habari zaidi.

YANGA: YANGA, VILLA BILA BILA



Mechi ya kirafiki na ya Kimataifa ya Sports Club Villakutoka Uganda na Dar es Salaam Young Africans ilimalizika 0-0 ndani ya uwanja wa Taifa....Mechi hii kwa Yanga ilikuwa ya kujiandaa na Kagame Cup na pia kutoa habari kuhusu mauwaji ya Albino yanayo endelea nchini...Mechi ilihudhuriwa na watu wengi akiwemo Waziri Mkuu Mizengo Pinda...Yanga pia walionyesha vifaa vyao vipya Donald Ngoma na Joseph Tetteh Zutah...Bofya hapa upate habari zaidi.

COPA AMERICA: BRAZIL NJE

Gonzalez
Brazil wametolewa kwenye Copa America na Paraguay kwenye matuta...Mchezaji wa zamani wa Manchester City Robinho aliwaweka mbele Brazil mapema dakika ya 15 lakini badaae kipindi cha 2 Thiago Silva alinawa mpira na Gonzalez alisawazisha bao la tuta...Brazil walifungwa 4-3 na kukumbusha mechi yao dhidi ya Paraguay mwaka 2011...Paraguay watacheza na Argentina tarehe 1 July...Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday 27 June 2015

COPA AMERICA: TEVEZ AIPELEKA ARGENTINA NUSU FAINALI


Bao la Carlos Tevez ndio lililowavusha Argentina mbele kwenye game dhidi ya Colombia...Argentina walishambulia sana lakini walikutana na kipa wa Arsenal ambae alikuwa makini sana kulinda lango...Ospina alizuia mashuti ya Lionel Messi, Sergio Aguero na Nicolas Otamendi....Game ilishia kwenye matuta na Tevez ndie aliepiga tuta la mwisho na kufanya Argentina washinde 5-4...Argentina wanasubiri kucheza na Brazil au Paraguay...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday 25 June 2015

KENYA: TIMU BINGWA YA VOLLEYBALL KUCHEZA WORLD GRAND PRIX


Timu ya taifa ya Kenya ya volleyball ambao ni mabingwa wa volleyball Afrika watacheza kwenye machindano makubwa sana ya volleyball duniani...Michuano hiyo inajulikana kama World Grand Prix na itafanyikia nchini Mexico...Hii ni mara ya 2 Kenya inahudhuria mashindano hayo makubwa duniani wanao leta mabingwa wote sehemu moja...Kenya imepangwa Group 3 pamoja na Algeria, Australia, Colombia, Cuba, Kazakstan, Mexico na Peru...Bofya hapa upate habari zaidi.

ORYX RALLY 2015: BAADHI YA PICHA ZA FINISH LINE

















COPA AMERICA: CHILE NDANI YA NUSU FINALI


Mauricio Isla ndiye aliyewapeleka Chile nusu fainali baada ya kupachika bao mwishoni...Chile waliwafunga Uruguay ambao walikuwa na watu 9 bao la pekee kutoka kwa Isla...Chile walicheza mpira safi na kuwakabili Uruguay bila ubishi...Vifaa viwili, Arturo Vidal na Eduardo Vargas, vilikuwa matata sana katika lango la Uruguay kabla ya Edison Cavani kutolewa nje na kadi nyekundu...Chile sasa wanasubiri kucheza na mshindi wa game ya kesho kati ya Bolivia na Peru...Bofya hapa upate habari zaidi.

Wednesday 24 June 2015

LIVERPOOL: ROBERTO FIRMINO NDANI YA THE KOP


Liverpool wamemsajili forward wa Hoffenheim, Roberto Firmino, kwa kiasi cha pound milioni 29...Firmino ni mbrazil ambae ni matata sana anayechezea timu ya taifa ya Brazil...Dogo mwenye umri wa miaka 23 anategemewa kukaa Anfield kwa miaka 5...Firmino akitoka Chile kwenye Copa America atafanyiwa uchunguzi wa afya na baada ya hapo ataingia the Kop...Bofya haa upate habari zaidi.

Tuesday 23 June 2015

ARSENAL: PETR CECH MBIONI KUINGIA EMIRATES


Kipa wa Chelsea kwa miaka 11 Petr Cech yuko mbioni kusajiliwa na Arsenal...Atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa Emirates kipindi cha usajili...Bofya hapa upate habari zaidi.

SIMBA S.C: DYLAN KERR KOCHA MPYA MSIMBAZI


Simba Sports Club sasa imepata mwanga baada ya kumchukua kocha wa anayetoka Uingereza Dylan Kerr...Kerr anachukua nafasi ya Goran Kopunovic...Aveva amesema wamefikia uamuzi mzuri na atakaa mwaka 1 na anaingia uwanjani Jumatatu kuanza mazoezi ya kujitayarisha na ligi ya mwaka 2015/2016...Bofya hapa upate habari zaidi.

JUVENTUS: MARIO MANDZUKIC NDANI YA JUVE


Star wa Atletico Madrid, Mario Mandzukic, ametia timu Juve...Juve wamenyakua Mandzukic wa milioni 13.6...Aliwafungia Atletico mabao 20 katika games 43 na aliingia Atletico kutoka Bayern Munich mwaka jana...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday 21 June 2015

BRAZIL: NEYMAR AFUNGIWA COPA AMERICA


Mchezaji maarufu wa Brazil Neymar, Jr. amefungiwa mechi 4...Neymar atakosa mechi zote za Copa America baada ya kupatikana na hatia ya kufanya fujo...Kwanza Neymar alipewa kifungo cha game moja alivyopata kadi nyekundu kwenye game yao na Colombia...Pili aliongezewa adhabu kutokana na Shirikisho la Soka Amerika ya Kusini kuangalia tena fujo zake ambazo inasemekana alichapa mchezaji na mpira baada ya mechi kuisha na badae akamgonga kichwa mchezaji mwingine na badae akazozana na refa kabla ya kwenda chumba cha kubadili nguo...Bofya hapa upate habari zaidi.

Wednesday 17 June 2015

EPL: FALCAO KARIBU ANAINGIA DARAJANI


Radamel Falcao yuko mbioni kuingia Chelsea kwa mkopo wa msimu mzima...Falcao ambae ameifungia mchezaji wa Monaco ambae ameifungia Manchester United mabao 29 ataingia Chelsea baada ya Man U kukataa kumchukua kwa milioni 43.2 pounds za Uingereza...Falcao sasa yuko anacheza kwenye Copa America huko Chile chini ya bendera ya Colombia...Bofya hapa upare bahari zaidi.

Sunday 14 June 2015

EUROPIAN CHAMPIONSHIP: RATIBA YA MECHI ZA LEO (GMT)

  • SloveniavEngland17:00
  • UkrainevLuxembourg17:00
  • BelarusvSpain19:45
  • SlovakiavMacedonia19:45
  • EstoniavSan Marino17:00
  • LithuaniavSwitzerland19:45
  • LiechtensteinvMoldova17:00
  • RussiavAustria17:00
  • SwedenvMontenegro19:45

GHANA: AYEW NDANI YA SWANSEA CITY


Andre Ayew mtoto wa aliyekuwa mkali wa soka Ghana Abedi Pele ameingia Swansea kwa free transfer kutoka Marseille...Ayew mwenye miaka 25 atakaa Swansea miaka 4...Ayew alikaa Marseille toka 2006 na amewafungia mabao 52 katika mechi 181 alizocheza pamoja na hayo ameichezea timu yake ya taifa mara 62...Bofya hapa upate habari zaidi.

Wednesday 10 June 2015

FIFA: POLISI WACHUKUA KOMPYUTA ZA FIFA


Fifa wametoa kumbukumbu zao za kielktroniki na kompyuta zao kwa polisi wa Uswisi kutokana na uchunguzi unaoendelea...Fifa iko kwenye uchunguzi wa kula rushwa na uchunguzi ambao umekamata wakurugenzi kadhaa wa sasa na wazamani...Polisi pia wamebeba kumbukumbu za aliyekuwa rais wa Fifa Sepp Blatter...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday 7 June 2015

CHAMPIONS LEAGUE 2015: BARCELONA MABINGWA WA SOKA ULAYA


Barcelona wakiwa ndani ya Olympic Stadium jijini Berlin walinyakua ubingwa wa Champion League mbele ya dunia nzima...Barcelona wanashinda kombe hilo kubwa kuliko yote Ulaya kwa mara ya 5 sasa...Barca kabla ya dakika tano za mwanzo walipiga gonga za akili na kupata bao safi kupitia kwa Rakitic...


Barca walishinda 3-1 kwa kucheza mpira wa akili na wa kasi ingawa Juve nao kipindi cha 2 walijitahidi sana na kuambulia bao lao la pekee kupitia kwa Morata dakika ya 55...Bofya hapa upate habari zaidi. 

F1: HAMILTON APATA AJALI CANADA


Bingwa wa mashindano ya magari ya Formula One Lewis Hamilton amepata ajali huko Canada...Hamilton alikongoza practice ya 2 lakini gari iliingia kwenye kingo mvua ilivyoanza...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday 1 June 2015

EPL: PATRICK VIEIRA YUKO KWENYE LIST YA KUWA KOCHA NEWCASTLE


Mchezaji wa zamani wa Arsenal na Manchester City Patrick Vieira yuko kwe list ya watu wanne wanaotarajiwa kuifundisha Newcastle United...Vieira ambae alishinda vikombe 3 vya ligi na FA Cup 4 akiwa na Arsenal kabla ya kusogea Juventus mwaka 2005 na badae kurudi Uingereza na kuichezea Manchester City mwaka 2010 na kuwasaidia wachukue kombe la FA mwaka 2011...Newcastle wamekaa bila kocha wa kudumu kwa muda toka Alan Pardew ajiunge na Crystal Palace...Bofya hapa upate habari zaidi.