Saturday 31 October 2015

VODACOM PREMIER LEAGUE: AZAM KILELENI BAADA YA KUICHAPA JKT RUVU


Azam imefanikiwa kuipita Yanga na kukaa kileleni baada ya kuichapa JKT Ruvu 4-2 ndani ya uwanja wa Karume...Ilichukua dakika 7 tu kupitia Didier Kavumbagu na John Bocco kuiweka Azam mbele lakini badae Najim Magulu alipata bao kabla ya half-time...Bofya hapa upate habari zaidi.

RUGBY WORLD CUP 2015: ALL BLACKS WAKO TAYARI KUWEKA HISTORIA


Leo ni leo bingwa wa Rugby duniani atajulikana kwenye fainali ya Rugby World Cup 2015 kati ya New Zealand na Australia ndani ya Twickenhan...New Zealand wanataka kuwa timu pekee ambayo itakuwa imeshinda kombe la dunia mara 2...


Itakuwa mara ya kwanza All Blacks na Australia wanakutana kwenye fainali na ukizingatia All Blacks wamepoteza mechi 3 tu kati ya 53 toka wanyanyue Webb Ellis Cup mwaka 2011 mechi ya fainali itakuwa kali sana...


Usikose fainali hii ambayo itaanza kurushwa live kuanzia 16:00 GMT...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday 30 October 2015

TANZANIA SWIMMING ASSOCIATION: TIMU YA SMWIMMING ITAENDA MICHUANO YA ZONE 3



TSA wamesema watapeleka timu ya swimmers kwenye michuano ya Zone III Invitational International Championship ambayo yanatarajiwa kuanza December 11 mpaka 13 jijini Kampala Uganda...Pamoja na kuhudhuria michuano hiyo pia ni muhimu sana kwa matayarisho ya Olympics za mwaka 2016 Rio de Janeiro...Bofya hapa upate habari zaidi.

F1: BINGWA WA DUNIA MARA 3 LEWIS HAMILTON ANATAKA GP YA AFRIKA YA KUSINI IRUDISHWE



Lewis Hamilton ambae ni bingwa wa dunia wa mashindano ya F1 amesema angefurahia kama wangeirudisha GP ya Afrika Kusini...Afrika ya kusini imechezesha mashindano hayo mara 23 toka 1962 mpaka 1993...


Lewis Hamilton alikuwa mtu wa kwanza mwenye asili ya kiafrika kushinda F1 mwaka 2007 na sasa ameshinda ubingwa wa dunia mara 3 pamoja na kushinda mashindano 43 mbali mbali...Bofya hapa upate habari zaidi.

WTA FINALS: SHARAPOVA AMCHAPA PENNETTA



Maria Sharapova amefanikiwa kumchapa Flavia Pennetta 7-5 6-1 na kuingia nusu fainali ya michuano hiyo ya WTA huko Singapore...Pennetta amesema huu ni msimu wake wa mwisho wa kucheza tennis...Serena Williams hakucheza kwenye fainali hizi kutokana na majeraha...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: RATIBA YA MECHI ZA WEEKEND (GMT)

Sat 31 Oct 2015
  • Chelsea v Liverpool 12:45
  • Crystal Palace v Man Utd 15:00
  • Man City v Norwich 15:00
  • Newcastle v Stoke 15:00
  • Swansea v Arsenal 15:00
  • Watford v West Ham 15:00
  • West Brom v Leicester 15:00
Sun 1 Nov 2015
  • Everton v Sunderland 13:30
  • Southampton v Bournemouth 16:00

Wednesday 28 October 2015

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA LEO

Position Team Played Goal Diff  Points
 1 Man City 10 16 22
 2 Arsenal 10 10 22
 3 West Ham 10 9 20
 4 Man Utd 10 7 20
 5 Leicester 10 3 19
 6 Tottenham 10 8 17
 7 Crystal Palace 10 1 15
 8 Southampton 10 3 14
 9 Liverpool 10 -2 14
 10 West Brom 10 -3 14
 11 Everton 10 0 13
 12 Swansea 10 0 13
 13 Watford 10 -2 13
 14 Stoke 10 -3 12
 15 Chelsea 10 -4 11
 16 Norwich 10 -7 9
 17 Bournemouth 10 -10 8
 18 Sunderland 10 -8 6
 19 Newcastle 10 -10 6
 20 Aston Villa 10 -8 4

FIFA: WATU 7 KUCHUANA NAFASI YA JUU YA URAIS


Fifa wametoa majina 7 ambayo yatachuana February 26 kuwania nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Duniani...Majina hayo ni Jerome Champagne, Gianni Infantino, Michel Platini, Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Prince Ali bin al-Hussein, Musa Bility na Tokyo Sexwale...Sepp Blater amesema atajiuzuru lakini sasa kasimamishwa kutokana na uchunguzi...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday 27 October 2015

CHAD: RIGOBERT SONG KOCHA MPYA


Chad wamechagua kocha mpya baada ya kumfukuza kocha kutokana na kushindwa kufuzu...Rigobert Song anakuwa kocha mpya wa Chad kutokana na uzoefu wake katika soka Afrika...Song amecheza Nations Cup mara 33 na ni rekodi pia ameshinda mara 2 kama captain mwaka 2000 na 2002...Amecheza World Cup mara 4 mwaka 1994 1998 2000 na 2010...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday 25 October 2015

AC MILAN: DOGO WA MIAKA 16 ACHEZA KWA MARA YA KWANZA


Kocha wa AC Milan, Sinisa Mihajlovic, aliamua kumchezesha dogo, Donnarumma, mwenye umri wa miaka 16 baada ya kuona hawapati ushindi katima mechi 3 za awali...Dogo huyo alicheza game kati ta AC Milan na Sassuolo...AC Milan sasa wamepanda nafasi ya 10...Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday 24 October 2015

Thursday 22 October 2015

EUROPA LEAGUE: RATIBA YA MECHI ZA LEO (GMT)

Wednesday 21 October 2015

CHAMPIONS LEAGUE: RATIBA YA MECHI ZA LEO (GMT)

CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL YAICHAPA BAYERN KWA AKILI



Aresenal jana walifanikiwa kupata mwanga walipowachapa Bayern Munich 2-0 ndani ya Emirates...Giroud ambae alikuwa sub kwenye dakika ya 77 alipachika bao la karibu baada ya kipa Manuel Neuer kufanya makosa...Mesut Ozil dakika za lala salama aliweza kupokea cross kutoka kwa Hector Bellerin na kupachika bao safi...Bayern walishikilia mpira muda mwingi na pia pasi zao zilikuwa za uhakika (90.7% ya pasi zilifika) ukilinganisha na Arsenal 74.5% lakini Arsenal ilibidi watumie akili ili waweze kushinda mechi hiyo ngumu na kipa pia alikuwa msaada sana...


Arsene Wenger amekuwa kocha wa kwanza kumchapa Pep Guardiola akiwa na Barcelona na Bayern kwenye Champions League...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday 20 October 2015

EPL: MSIMAMO WA LIGI

Position Team Played Goal Dif  Points
 1 Man City 9 16 21
 2 Arsenal 9 9 19
 3 Man Utd 9 7 19
 4 West Ham 9 8 17
 5 Leicester 9 2 16
 6 Crystal Palace 9 2 15
 7 Tottenham 9 4 14
 8 Southampton 9 3 13
 9 Everton 9 1 13
 10 Liverpool 9 -2 13
 11 Stoke 9 -1 12
 12 Chelsea 9 -3 11
 13 West Brom 9 -4 11
 14 Swansea 9 -1 10
 15 Watford 9 -4 10
 16 Norwich 9 -6 9
 17 Bournemouth 9 -6 8
 18 Newcastle 9 -7 6
 19 Aston Villa 9 -7 4
 20 Sunderland 9 -11 3

RUGBY WORLD CUP 2015: REFA ALIKOSEA KUTOA PENALTY YA SCOTLAND



Refa aliyesimamia mechi kati ya Australia na Scotland alikosea kutoa penalty mwishoni kabisa...World Rugby walisema refa huyo ambae ni Craig Joubert alikosea kutoa penalty na angetoa Scrum kwa Australia baada ya Nick Phipps kugusa mpira awali...Scotland walifungwa 35-34...Bofya hapa upate habari zaidi.

CHAMPIONS LEAGUE: RATIBA YA MECHI ZA LEO (GMT)


Monday 19 October 2015

EPL: NEW CASTLE YAONA MWEZI YAMCHAPA NORWICH 6-2


New Castle hatimaye wameweza kufunga na wamefunga kwa mabao kibao...Georginio Wijnaldum alekuwa star wa mchezo baada ya kupachika mabao 4 kati ya mabao 6 waliofungwa Norwich...



New Castle ndio wanapata ushindi wao kwanza kabisa msimu huu na wametoka eneo la hatari kwenye msimamo wa ligi...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday 18 October 2015

RUGBY WORLD CUP 2015: AUSTRALIA YASHINDA MECHI KALI DHIDI YA SCOTLAND


Australia wameshinda mechi kali na muhimu ya robo fainali ya Rugby dhidi ya Scotland...Australia walishinda 35-34 kupitia mpira wa penalty ya utata dakika ya mwisho kabisa kupitia kwa Bernard Foley...



Intetception ya Mark Bennet wakati imebakia dakika 7 tu ilikuwa imewaweka Scotland mbele lakini mambo yaliibadilika muda si mrefu... Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday 17 October 2015

NBA: LAMAR ODOM AZINDUKA KUTOKA KWENYE COMA



Mchezaji maarufu wa basketball wa zamani Lamar Odom ametoka kwenye coma...Odom aliweza kumsalimia mke wake, Khloe Kardashian, ambae wanapitia zoezi la kuachana, kwa kumwambia 'Hi'...Odom alikutwa kazimia ndani ya danguro moja jijini Las Vegas Marekani na sasa anapambana apone lakini inasemekana organs zake nyingi hazifanyi kazi...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday 16 October 2015

ROTARY MARATHON 2015: ZAIDI YA SHILING BILIONI 1 ZAPATIKANA


Mdau wa Max Sports wakili maarufu Anthony Mark akiwa amemaliza 21km

Rotary Club 6 za Dar es Salaam wakishirikiana na wafadhili wengine wameweza kupata zaini ya Shilingi bilioni 1 ambazo zitaenda kusaidia kujenga sehemu ya matibabu hapa jijini Dar...Rotary Marathon ilifadhiliwa na Bank M pamoja na wadau wengine na mgeni rasmi alikuwa Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi...

 
Mdau wa Max Sports mjasiriamali Evans Nyeme (Wa 3 kushoto)

Wadau walioweza kuhuthuria walikuwa zaidi ya 13,000 wakiwemo wadau wa Max Sports, watoto, wakina mama, na wasiojiweza...Mzee Mwinyi amesema juhudi za Rotary za kusaidia jamii lazima zijulikane na pia yeye amehudhuria marathon toka 2009 na amesema marathon imesaidia kuimarisha maisha ya wakazi wengi...Bofya hapa upate habari zaidi.

FIFA: UEFA YAMUUNGA MKONO PLATINI



UEFA imesema inamuunga mkono Platini na inataka apewe nafasi ya kujitetea na kifungo chake cha siku 90 kimalizike aendelee na mambo mengine...Pamoja na kuungwa mkono sasa amejitokeza mtu mwingine ambae anataka kiti cha urais wa FIFA...Sheikh Salman bin Ibrahim Al Khalifa nae karibu atatangaza kuingia kwenye kinyan'ganyiro cha kutafuta rais mpya wa FIFA...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday 15 October 2015

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

Position Team Played Goal Diff Points
1 Man City 8 12 18
2 Arsenal 8 6 16
3 Man Utd 8 4 16
4 Crystal Palace 8 4 15
5 Leicester 8 2 15
6 West Ham 8 6 14
7 Everton 8 4 13
8 Tottenham 8 4 13
9 Southampton 8 3 12
10 Liverpool 8 -2 12
11 Swansea 8 0 10
12 Watford 8 -1 10
13 Norwich 8 -2 9
14 Stoke 8 -2 9
15 Bournemouth 8 -2 8
16 Chelsea 8 -5 8
17 West Brom 8 -5 8
18 Aston Villa 8 -5 4
19 Sunderland 8 -10 3
20 Newcastle 8 -11 3

EPL: RATIBA YA MECHI ZA WEEKEND (GMT)

Sat 17 Oct 2015
  • Tottenham v Liverpool 12:45
  • Chelsea v Aston Villa 15:00
  • Crystal Palace v West Ham 15:00
  • Everton v Man Utd 15:00
  • Man City v Bournemouth 15:00
  • Southampton v Leicester 15:00
  • West Brom v Sunderland 15:00
  • Watford v Arsenal 17:30
Sun 18 Oct 2015
  • Newcastle v Norwich 16:00

Wednesday 14 October 2015

NBA: LAMAR ODOM AKUTWA AMEZIMIA NDANI YA DANGURO


Lamar Odom mchezaji wa zamani wa LA Lakers amekutwa amezimia akiwa ndani ya danguro jijini Las Vegas...Habari zinazotoka huko zinasema alikutwa kifudifudi na alipogeuzwa alitapika sana...Polisi waliitwa eneo la tukio na pia watu wa emergency medicine wakuwepo na walijaribu kumweka kwenye helicopter lakini hakuweza kuingia kutokana na urefu wake...Walimkimbiza na ambulance kumpeleka hospitali...



Lamar alikuwa ameoa kwenye familia maarufu sana ya Kardashians...Waliachana na mke wake Khloe muda si mrefu lakini mke huyo wa zamani yuko nae hospitalini na anamwombea apone...Max Sports tunamwombea Lamar apone haraka...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday 13 October 2015

MBWANA SAMATTA: NDANI YA LIST LA MCHEZAJI BORA AFRICA



Tanzanian International Mbwana Samatta amechaguliwa kwenye orodha ya wachezaji bora Africa...CAF wametoa list ya wachezaji 24 na Tanzania kwa mara ya kwanza iko kwenye list hiyo...Samatta ambae anachezea TP Mazembe ameisaidia timu hiyo kufika fainali za CAF Champions League mwaka huu na aliweza kupata mabao 6...Pia mchezaji wa Simba ameisaidia Tanzania kuwapita Malawi kwenye maandalizi ya 2018 FIFA Worod Cup...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday 12 October 2015

NFL: GIANTS YAFANYA MAMBO MWISHONI


New York Giants quarter ya 4 waliweza kuwafunga San Fransisco 49ers baada ya Eli Manning kurusha mpira yadi 82 mbali ndani ya eneo la maadui zao na kudakwa na Larry Donnell na kushinda 30-27...Giants hawakuamini kwani wide receiver wao Odell Beckham Jr. alikuwa nje kwa majeraha na walikuwa wanajua hawana receiver mkali ndani...Giants sasa wanaongoza NFC East (3-2)...Bofya hapa upate habari zaidi.

CONTINENTAL CUP: MABINTI WA ARSENAL WAICHAPA BIRMINGHAM CITY 3-1


Arsenal upande wa wanawake wanaendelea vizuri na mpira baada ya kuwachapa Birmingham City 3-1...Arsenal wanaingia fainali ya Continental Cup kwa mara ya 5 mfululizo...Marta Corredera anayetokea Spain ndiye aliyefungulia mabao...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday 11 October 2015

TAIFA STARS: MALAWI WASHINDA 1


Taifa Stars leo wamechapwa 1 na Malawi ndani ya jiji la Blantire leo...Pamoja na kuchapwa tunasonga mbele kwani tulishinda 2-0 kwenye mechi ya awali nyumbani...Kazi kubwa iko tukipambana na timu kali ya Algeria katika mechi ijayo...Tanzania tulianza kwa kushambulia lakini mashambulizi hayakuzaa matunda na Malawi nao walishambulia na hatimaye wakapata bao...Bofya hapa upate habari zaidi.

CHINA OPEN FINAL: DJOKOVIC AMCHAKAZA NADAL


Novak Djokovic amechukua ubingwa wa ATP China Open kwa mara ya 6...Djokovic alifanya hivyo baada ya kumchapa vibaya sana mkongwe wa clay court Rafa Nadal 6-2 6-2...Kwa upande wa wanawake Gabrine Muguruza alishinda kwa kumchapa Timea Bacsinszky katika fainali ya WTA...Bofya hapa upate habari zaidi.

F1: LEWIS HAMILTON AMESOGEA KARIBU NA UBINGWA BAADA YA USHINDI RUSSIA


Lewis Hamilton ameshinda Russian GP na sasa yuko karibu na ubingwa wa mashindano haya makali ya magari ya formula one...Hamilton alikuwa wa pili nyuma ya mwenzake Nico Rosberg lakini badae Rosberg alipata matatizo ya gari yake...Sebastian Vettel wa Ferrari alichukua nafasi ya 2...Sergio Perez wa Force India alichukua nafasi ya 3 baada ya Kimi Raikkonen wa Ferrari kugongana vibaya na Valtteri Bottas kwenye lap ya mwisho...Bofya hapa upate habari zaidi.

LIVERPOOL: INTERVIEW YA KLOPP

 

Pata interview ya kocha mpya wa The Kop, Jurgen Klopp, alipokutana na waandishi wa habari...Klopp ametokea Burussia Dortmund na ametia saini mkataba wa miaka 3 kwa bei ya milioni 15 pound za Uingereza...

Friday 9 October 2015

LIVERPOOL: KLOPP ASEMA KAZI YAKE MPYA SIO RAHISI


Kocha mpya wa timu ya Merseyside Jurgen Klopp amesema kazi yake mpya nikazi ngumu katika ulimwengu wa mpira duniani...Klopp ameingia Liverpool kwa mkataba wa miaka 3 na atalipwa milioni 15 pounds za Uingereza...Klopp akiongea na LFCTV amesema yeye sio mtu wa vitu rahisi kwahio kazi mpya ni changamoto kubwa kwake...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday 8 October 2015