Wednesday 21 October 2015

CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL YAICHAPA BAYERN KWA AKILI



Aresenal jana walifanikiwa kupata mwanga walipowachapa Bayern Munich 2-0 ndani ya Emirates...Giroud ambae alikuwa sub kwenye dakika ya 77 alipachika bao la karibu baada ya kipa Manuel Neuer kufanya makosa...Mesut Ozil dakika za lala salama aliweza kupokea cross kutoka kwa Hector Bellerin na kupachika bao safi...Bayern walishikilia mpira muda mwingi na pia pasi zao zilikuwa za uhakika (90.7% ya pasi zilifika) ukilinganisha na Arsenal 74.5% lakini Arsenal ilibidi watumie akili ili waweze kushinda mechi hiyo ngumu na kipa pia alikuwa msaada sana...


Arsene Wenger amekuwa kocha wa kwanza kumchapa Pep Guardiola akiwa na Barcelona na Bayern kwenye Champions League...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment