Friday 30 May 2014

NBA: LA CLIPPERS YANUNULIWA NA MKURUGENZI WA ZAMANI WA MICROSOFT


LA Clippers yanunuliwa na aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa zamani wa Microsoft, Steve Ballmer, kwa billioni 2 dola za Marekani....Steve Ballmer ana BA ya Hisabati na Uchumi kutoka Harvard...Aliingia Microsoft 1980...Alikuwa CEO wa Microsoft 2000-2014...Bid ya Ballmer ilikuwa kubwa kuliko za wengine waliotaka kuinunua Clippers...Kwa bei ya billioni 2 Ballmer atakuwae tajiri mmiliki wa timu kuliko wengi marekani...Kwa ujumla Steve Ballmer anathamani ya bilioni 20...Bofya hapa upate mamb zaidi...

Thursday 29 May 2014

TEXAS A&M: SALIM JUMA ZONGO MTANZANIA ANAYEFANYA VIZURI HUKO MAREKANI

Salim Juma Zongo ni mtanzania anayeishi Marekani ambaye anacheza American Football na anaichezea timu ya Texas A&M (Lions) huko Texas Marekani...Zongo alizaliwa mwaka 1991... 


Alichukuliwa na kukaa na uncle (Mama yake Zongo ni dada mkubwa) ambae ni mdau mkubwa sana wa Max Sports, Rashid Mchujuko, mwaka 2000 na waliishi Washington DC...Baada ya hapo walihamia  Utah wakaishi kwa muda na hatimaye wlihamia Dallas, Texas...High School alichezea timu yake ya shule Fossil Ridge High School na huko alipata tuzo nyingi sana...



Stats za dogo kabla ya A&M zilikuwa kama hivi: pasi 33 katika yadi 528 akiwa senior...Zongo anachezea timu ya shule yake ya Texas A&M kama Wide Receiver...Dogo ni mkali sana na ameisaidia sana timu hiyo kubwa ya college football Marekani...


Kuna watanzania wengi wanafanya vizuri lakini hawafahamiki Max Sports inajitahidi kuwaletea habari za vijana wetu na wadau wa michezo duniani...


Tunakutakia heri Salim Juma Zongo kwenye masomo na maendeleo yako kwenye michezo na maisha kwa ujumla...

NBA: INDIANA PACERS WASHINDA GAME 5


Indiana Pacers wamejitahidi na kushinda game 5...Pacers walishinda 93-90...Miami walikuwa nyuma points 11 kipindi cha robo ya mwisho (4th quarter) lakini walicheza vizuri sana na kurudisha magoli mpaka wakawa point 1 tu nyuma...Wade alisaidia sana Miami kurudisha magoli...Pacers walikomaa mpaka dakika ya mwisho...Paul George ndio aliwainua sana Pacers na alimaliza na points 37....Sasa inabidi Pacers washinde game 6 kama kweli wanataka kuchukua ubingwa...Bofya hapa upate habari zaidi...

EPL: WENGER AKINGIWA KIFUA KUTUMIA PESA NYINGI



Arsene Wenger atkubaliwa kutumia pesa nyingi katika msimu wa usajili ingaawa Wenger sio mtu wa kutoa pesa nyingi kununua wachezaji...Rekodi ya Arsenal ni milioni 42.5 pounds za Uingereza kumnunua Mesut Ozil...Director Lord Harris kutoka Peckham aliwaambia gazeti la Times kwamba Arsene Wenger anaweza kuvunja rekodi ya kununua wachezaji msimu unaokuja...Pia bado Wenger hajasaini mkataba mpya na club lakini atasaini muda si mrefu...Bofya hapa upate mambo zaidi...

FRENCH OPEN: SERENA WILLIAMS NJE


Serena Williams ametolewa nje ya round ya 2 ya michuano mikali ya French Open baada ya kuchapwa na dogo Garbine Muguruza 6-2 6-2...Serena anamfuata dada yake Venus Willims aliyetolewa na Ana Schmiedlova 2-6 6-3 6-4...Sasa Muguruza mwenye miaka 20 ataakutaanaa na Schmiedlova kwenye round ya 3 ya michuano hiyo mikali sana...Hii ni mara ya kwanza kwenye historia Serena anatolewa mapema kwenye mechi kubwa Grand Slam...Hapo awali mkali mwingine Li-Na aliga mashindano mapema...Bofya hapa upate habari zaidi...

EPL: MMILIKI WA MANCHESTER UNITED WA AFARIKI



Malcom Glazer amefariki dunia akiwa anamiaka 86...Billionaire Malcom alinunua Manchester United kwa millioni 790 pounds za Uingereza lakini mashabiki hawakumpenda sana kwakuwa timu ilikumbwa na madeni mengi na kukwamisha shughuli nyingi za timu hiyo...Pamoja na kuchukiwa timu ilishinda Premiership 5 na Champions Legue 1 wakati akiwa mmiliki...2006 alipata Stroke na watoto wake wawili ndio walikuwa wanamsaidia katika shughuli zake za kila siku....Bado familia ya Glazer inamiliki asilimia 90% ya Manchester United ambayo kila mtoto wake ana asilimia 10%...Glazer pia alikuwa mmiliki wa timu ya American Football Tampa Bay Buccaneers...Alinunua Tampa Bay kwa millioni 192 dola za Marekani...Aliendelea kununua shares katika makambpuni mbalimbali yakiwemo Tonka, Harley Davidson, Houlihan's restaurants, Zapata Corporation na nyingine nyingi....Glazer ameacha mke na watoto 6 na wajukuu 14...Bofya hapa usome zaidi...

Tuesday 27 May 2014

FRENCH OPEN: DJOKOVIC ASONGA MBELE


Novac Djokovic amesonga mbele kwenye round ya kwanza ya michuano mikali ya French Open...Mechi iliyochukua saa 1 na dakika 46 Djokovic ambae ni Namba 2 duniani kwenye rankings za French Open aliweza kumshinda Joao Sousa 6-1 6-2 6-4 huko Rolan Garos...Raael Nadal pia aliweza kushinda mechi yake ya round ya kwanza dhidi ya Robby Ginepri kutoka Marekani....

Monday 26 May 2014

AFRICA YOUTH GAMES: TANZANIA YAICHAPA BOTSWANA


Tanzania inaendelea vizuri kwenye mashndao ya vijana ya Afrika huko Gabarone Botswana...Timu ya Tanzania U-15 aliichapa Bostwana 2-0 katika uwanja wa SSKB...Vijana wa Tanzania walicheza vizuri sana na game inayofuata ni dhidi ya Swaziland na Nigeria Jumanne na watamalizia na South Africa Alhamisi...Haya mashindano yanahusisha wanamichezo 2,500 kutoka nchi 54 kwa siku kumi...

NBA: IBAKA ARUDI KUISAIDIA OKC


Serge Ibaka ameamua kurudi kwenye Game 3 baada ya kuwa nje kutokana na kuumia...OKC walishinda Game 3 dhidi ya Spurs 106-97...Sasa Spurs wanaongoza kwa game 2 na OKC wameshinda 1...Ibaka alifanya vizuri kwenye Game 3 alipata points 15, rebounds 7 na blocks 4...Alitumia dakika 29 tu kufanya mambos...OKC walikuwa wanamhitaji sana Ibaka maana maji yalikuwa shingoni...Durant alipata points 25 na rebounds 10 wakati Westbrook alipata points 26, rebounds 8, assists 7 na steals 3...Pata mambo yalivyo kwenda mwanzo mwisho.

EPL: QPR WARUDI PREMIERSHIP


QPR wamerudi tena Premiership baada ya kuwachapa Derby 1-0...Kikosi cha watu 10 kiliweza kupata goli moja tu ambalo liliwawezesha kurudi kwenye top-flight football...Zamora dakika za mwisho ndiye aliyepachika bao bada ya beki Richard Keogh kufanya kosa...Bofya upate habari zaidi...

Sunday 25 May 2014

F1: NICO ROSBERG ASHINDA MONACO GP


Nico Rosberg aibuka mshindi huko Monaco....Rosberg alimshinda Lewis Hamilton na Ricciardo katika mashindano ambayo yalichangaamka badae na yalitoa safety cars mara mbili...

Perez akitoka kwenye gari baada ya kugongwa

Mara ya kwanza ilitokea mwanzoni wakati Button wa McLaren alimgonga Perez wa Force India....Hapo awali Lewis Hamilton alilalamika kuwa mwenzake Nico alicheza foul ili amzuie asiamze mbele ya grid...Lakini wasimamizi walisema ilikuwa bahari mbaya na ni kosa dogo...


Leo waliofanya vizuri ni Nico Rosberg, Lewis Hamilton, Ricciardo na Alonzo...Bofya hapa upate habari zaidi....

UEFA CHAMPIONS LEAGUE FINALS: REAL MADRID MABINGWA 2014


Real Madrid wamenyakua kombe kubwa sana la UEFA Champions League huko Lisbon, Portugal...Mabingwa hawa walichukua kombe mbele ya Zenadine Zidane ambaye alikuwa mchezaji wa Real Madrid wa zamani na kikosi chake ndicho kilichukua kombe mara ya mwisho...Mambo hayakuwa kama yalivyo tarajiwa lakini habari ndio hiyo na pia rafu zilikuwa nyingi na ngumi zilikuwa karibu zichapwe mara nyingi...Refaalijitahidi sana kuweka mambo sawa...



Atletico walikuwa makini sana kipindi cha kwanza lakini walichemsha na kumwingiza Diego Costa ambae ni majeruhi na hakukaa sana akatolewa...Lakini baada ya hapo Atletico walicheza mpira sana na kuwakabili Real...Real Madrid walianza kwa uoga na mpira wao ulikuwa sio wadau walivyowazoeakuwaona wakicheza...Mnamo dakika ya 36 Diego Godin aliwaweka Atletico mbele...Baada ya kipindi cha pili Real Madrid walianza kucheza kama kawaida yao lakini beki wa Atletico walikuwa makini sana kupangua mambo...



Kipa wa Atletico alifanya kazi kubwa sana na pia kutokana na urefu wake alipangua sana mashuti hatari kutoka kwa Ronaldo na wenzake...Mechi ilikuwa ya Atletico lakini dakika ziliongezwa nyingi na dakika ya 93 Sergio Ramos alipata bao zuri na kuwapa matumaini Real Madrid...Baada ya Bale kupachika bao lingine Atletico walisambaratika....Marcelo na Ronaldondi wakamaliza mchezo...Bofya hapa upate mambo zaidi yalivyokuwa...

Saturday 24 May 2014

SOCCER: RICHEST DEFENDERS IN THE WORLD

Player From To Amount (£m) Date
Thiago Silva
AC Milan
Paris St-Germain
36
2012
Rio Ferdinand
Leeds United
Manchester United
33.1
2002
Marquinhos
Roma
Paris St-Germain
27
2013
Fabio Coentrao
Benfica
Real Madrid
27
2011
Pepe
Porto
Real Madrid
25
2007




























EPL: DAVID LUIZ ANYAKULIWA NA PSG


David Luiz amechukuliwa na Paris St-Germain kwa pound za Uingereza milioni 40...Beki huyu mkali kutoka Brazil alichukuliwa na Chelsea kutoka Benfica mwaka 2011 kwa pound za Uingereza millioni 21.3...Barcelona walikuwa wanataka huyu dogo lakini alishindwa kumchukua...PSG wameamua kutumia msuli wa pesa kumchukua dogo...Ingawa kocha wa Chelsea, Jose, alikuwa hamtumii sana dogo kama kikosi cha kwanza cha mabeki lakini dogo ni mzuri na atawasaidia sana PSG...Bofya hapa upate mambo zaidi...

GOLF: THOMAS BJORN AWEKA REKODI BMW PGA CHAMPIONSHIP


Thomas Bjorn aliweza kuweka rekodi kwenye round ya kwanza ya BMW PGA Championship...Bjorn alipata birdies 8 na eagle 1 na kumalizia na score ya 62...Bofya hapa ufuatilie zaidi kuhusu PGA Championship...

Friday 23 May 2014

NBA: MSIMU WA KUCHAGUA VIJANA KUTOKA VYUO VIKUU

NBA draft ni tukio la kila mwaka ambalo vijana wakali sana kwenye basketball na wanaotaka kuinga NBA wanachaguliwa na kusajiliwa na NBA...Lakini lazima wamalize miaka minne ya shule ili waweze kukubaliwa kama hawataki basi itabidi wakubali kuacha shule na kusajiliwa NBA...Timu zinazosajili zinapangwa kutokana na jinsi zilivyo fanya msimu uliopita....Timu zilizofnya vibaya vinapewa nafasi kubwa ya kuchagua kwanza ili wapate wachezji wazuri...Hii yote inafanyika kwenye lottery ambayo timu zote ambazo hazijaingia kwenye playoffs zinaingizwa kwenye lottery ambayo ina round 2...Hapo chini ni mpangilio wa timu zitazochagua wachezaji hao wapya round ya kwanza....

 
1. Cleveland Cavaliers
 
2. Milwaukee Bucks
 
3. Philadelphia 76ers
 
4. Orlando Magic
 
5. Utah Jazz
 
6. Boston Celtics
 
7. Los Angeles Lakers
 
8. Sacramento Kings
 
9. Charlotte Hornets
(From Detroit)

 
10. Philadelphia 76ers
(From New Orleans)

 
11. Denver Nuggets
 
12. Orlando Magic
(From New York via Denver)

 
13. Minnesota Timberwolves
 
14. Phoenix Suns
 
15. Atlanta Hawks
 
16. Chicago Bulls
(From Charlotte)

 
17. Boston Celtics
(From Brooklyn)

 
18. Phoenix Suns
(From Washington)

 
19. Chicago Bulls
 
20. Toronto Raptors
 
21. Oklahoma City Thunder
(From Dallas via HOU & LAL)

 
22. Memphis Grizzlies
 
23. Utah Jazz
(From Golden State)

 
24. Charlotte Hornets
(From Portland)

 
25. Houston Rockets
 
26. Miami Heat
 
27. Phoenix Suns
(From Indiana)

 
28. Los Angeles Clippers
 
29. Oklahoma City Thunder
 
30. San Antonio Spurs

Thursday 22 May 2014

YATCH RACING: MABAKI YA BOTI YA 'CHEEKI RAFIKI' ILIYOPOTEA YA BAHARI YA PASIFIC


Boti kubwa ya futi 40 ya mashindano ya regatta iliyopotea huko bahari ya Pacific yapatikana mabaki machache tu...Boti hiyo iliyokuwa inaitwa Cheeki Rafiki kutoka Uingereza ilishiriki mashindano huko Antigua na ilikuwa inarudi nyumbani ilipopotea...Boti hiyo ilikuwa inatafutwa sana na jumamosi iliyopita walikata tamaa na kuacha kuitafuta lakini Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza iliweka msisitizo mkali na jumanne wakaendelea kuitafuta...Zimetumika ndege 3 na meli 6 kwenye eneo ambalo inasemekana hiyo boti ilipotea au kuzama maili 1,000 kutoka Cape Cod, Massachusetts, huko Marekani...Boti hiyo ilipotea ikiwa na watu wa nne tu...Bofy hapa upate habari zaidi...

F1: MSIMAMO WA MASHINDANO YA F1 MAKA SASA