Sunday 4 May 2014

BOXING: FLOYD MAYWEATHER ASHINDA KWA POINTS


Pambano kali la mabingwa lililofanyika huko MGM Grand Marekani lilisha kwa ushindi wa Floyd Mayweather dhidi ya Maidana..Floyd sasa ni bingwa wa WBA na WBC...Round za mwanzo Maidana alimsumbua sana Mayweather na Mayweather alikuwa anavuta pumzi tu...Maidana aliweza kuzichapa vizuri na alirusha makonde mengi lakini mengine hayakufika...


Round zote 5 zilikuwa za Maidana...Floyd ilibidi aanze kutumia ujuzi na akaanza kubadilisha mchezo baada ya Maidana kupunguza kasi...Inasemekana hakuna mtu aliyewahi kutupa makonde mengi kama Maidana na anasema anataka kuzichapa tena na Floyd...Round ya 4 waligongana vichwa na Floyd alikuwa analalamika sana...Alisema round mbili baada ya kugongana alikuwa haoini lakini alivyo anza kuona alichangamka na kuzichapa...Score card ya majaji ilikuwa 114-114, 117-111 na 116-112...Bofya hapa upate habari zaidi...


No comments:

Post a Comment