Sunday 4 May 2014

EPL: ARSENAL YASHEREHEKEA NAFASI CHAMPIONS LEAGUE


Arsenal imesherehekea nafasi yakuingia Champions League baada ya kumchapa West Brom 1-0..Baada ya Everton kuchapwa na Manchester City jana ushindi wa leo umewapa uhakika wa kuingia Champions League..West Brom watahakikishiwa kubakia kwenye Premiership kama Norwich watachapwa na Chelsea....Game ya leo ilikuwa rahisi kwa Arsenal kwani defense ya Arsenal haikuhangaika kabisa...Kwenye dakika ya 14 goli pekee la mchezo wa leo lilitoka kwa Giroud baada ya kona iliyopigwa na Santi Carzola...Arsenal hawajawahi kukosa kucheza Champions League toka Arsene Wenger aingie kama kocha...

No comments:

Post a Comment