Friday, 2 May 2014

F1: WATU WENGI WAJITOKEZA KWENYE KUMBUKUMBU YA MIAKA 20 YA KIFO CHA AYRTON SENNA


Maelfu ya watu wamejikokeza Imola Circuit kutoa heshima zao kwa dereva wa mashindano ya F1 ambaye alikuwa bingwa wa dunia na mfano wa kuigwa katika ulimwengu wa mashindano ya magari...


Ayrton Senna da Silva kutoka Brazil alifariki kwa ajali miaka 20 iliyopita kwenye kona moja kali wakati yuko kwenye mashindano huko Imola, Italy...



Senna inasemekana alikuwa dereva bora kuliko wote kipindi hicho na wengi wamemuenzi.

Senna alifariki akiwa na miaka 34 tu lakini alikuwa maarufu sana miaka hiyo.

Alonzo ambae ni dereva wa F1 sasa alikuwa mmoja wa watu waliohudhuria ukumbusho huo.

Alonzo alisema Senna alikuwa anapendwa na watoto wengi na ukiona helmet ya njano yenye namba 1 ujue huyo ni Senna anafanya vitu vyake.


Ron Dennis CEO wa McLaren ambae alikuwa team principal wakati Senna anashinda ubingwa wa dunia 1988 alisema Senna aliishi kwa ajili wa mchezo huo na watu wakifanya hivyo wanaacha vitu vyote na wanakuwa bora kwa hicho kitu.



Watu walikaa kimya kwa heshima 13:17 BST muda Senna alioaga dunia.

Pia siku moja kabla ya kufariki Senna alifariki dereva mwingine Ronald Ratzenberger kwenye hiyo hiyo circuit...Wote walikumbukwa jana.

Watu waliweka maua sehemu walizopata ajali.

Senna atakumbukwa daima kwa mchango wake ndani na nje ya F1...Bofya hapa upate habari zaidi za Senna






No comments:

Post a Comment