Tuesday 6 May 2014

EPL: MBIO ZA UBINGWA ZA LIVERPOOL ZAISHIA UKINGONI


Kilichotokea jana kiliacha midomo wazi kwa wadau wa Liverpool na wadau wa soka duniani baada ya kuona Liverpool wakiachia magoli matatu yaingie wakati zilmebaki dakika 11 mpira uishe...Yalikuwa majonzi tu kwa supa staa wa Liverpool Suarez maana ubingwa ndio umeota mbawa...Liverpool walianza kwa makeke yakushambilia hapa na pale na ikazaa matunda wakati Joe Allen, Sturridge na Suarez kupachika mabao na kuwa na nafasi nzuri ya kuwashinda Crystal Palace lakini mambo hayakuwa mambo baada ya mabeki kuamua kula yale matunda...Hatujui kama walilala au walikuwa wanawaza kombe maana dakika za mwisho Crystal Palace waliweza kurudisha mabao yote matatu kupitia Damien Delaney na substitute Dwight Gayle ambae alipachika mawili...Baada ya hapo yalikuwa majonzi tu...

Suarez kaagusha kilio (hiii  hiii ....siamini...hiii)...Bofya hapa upate habari ya defence mbovu ya Liverpool...

No comments:

Post a Comment