Monday 12 May 2014

EPL: MANCHESTER CITY MABINGWA


Hatimaye kapatikana bingwa kwenye ligi inayofuatiliwa sana duniani ya English Premiership...Bingwa huyo ni Manchester City....Liverpool hawakuwa nyuma sana lakini walizidiwa na hawakuweza kutunza points zao...Manchester City kama mnavyokumbuka ilikuwa timu ambayo ilitumia pesa nyingi kusajili wachezaji miaka michache iliyopita na sasa imezaa matunda...


Mwafrika Yaya Toure ametokea kuwa mchezaji safi na makini na amewasaidia sana City kuutwaa ubingwa mwaka huu...Msimu huu ulikuwa mgumu sana kwa timu zote na ushindani ulikuwa mkubwa sana na sasa itabidi timu zikajipange upya kwa mshimu ujao...Max Sports na wadau tunawapa hongera Manchester City kwa kuwa mabingwa tena kwa mara ya 5...

No comments:

Post a Comment