Sunday 18 May 2014

FA CUP: ARSENAL MABINGWA FA CUP 2014


Arsenal hatimaye wameshinda kombe la FA.

Ni miaka 9 toka Arsenal washinde na ushindi huu umeonyesha uvumilivu wa kocha na club kwani miaka ilikuwa inasonga tu.

Baada ya ushindi Arsene Wenger alienda upande wa mashabiki wa Arsenal ambao walikuwa na furaha sana.

Haya mambo yalianza sivyo kwa Arsenal kwani ndani ya dakika 9 tu walikuwa chini mabao 2.


Bao la kwanza alifunga Chester na la pili alifunga Davies.

Hull waliwachanganya mabeki na kujihakikishia nasafasi ya kulinda hayo magoli.

Arsenal walikuwa wanajaribu sana kushambulia ili warudishe lakini ilikuwa ngumu.

Mnamo dakika ya 17 free-kick kali sana iliyopigwa na Santi Carzola ilizaa matunda.

Arsenal iliendelea kushambulia lakini half-time ubao ulisoma 2-1.


Dakika ya 71 ilipigwa kona na Sagna aliirukia kwa kichwa ikamkuta Koscielny na kuipachika, mpira ulimalizika 2-2.

Dakika ya 109 kwnye muda ulioongezwa Ramsey akifunga goli zuri sana na hapo defense ya Hull ikaparanganyika kabisa...Bofya upate mambo zaidi hapa.

No comments:

Post a Comment