Thursday 29 May 2014

TEXAS A&M: SALIM JUMA ZONGO MTANZANIA ANAYEFANYA VIZURI HUKO MAREKANI

Salim Juma Zongo ni mtanzania anayeishi Marekani ambaye anacheza American Football na anaichezea timu ya Texas A&M (Lions) huko Texas Marekani...Zongo alizaliwa mwaka 1991... 


Alichukuliwa na kukaa na uncle (Mama yake Zongo ni dada mkubwa) ambae ni mdau mkubwa sana wa Max Sports, Rashid Mchujuko, mwaka 2000 na waliishi Washington DC...Baada ya hapo walihamia  Utah wakaishi kwa muda na hatimaye wlihamia Dallas, Texas...High School alichezea timu yake ya shule Fossil Ridge High School na huko alipata tuzo nyingi sana...



Stats za dogo kabla ya A&M zilikuwa kama hivi: pasi 33 katika yadi 528 akiwa senior...Zongo anachezea timu ya shule yake ya Texas A&M kama Wide Receiver...Dogo ni mkali sana na ameisaidia sana timu hiyo kubwa ya college football Marekani...


Kuna watanzania wengi wanafanya vizuri lakini hawafahamiki Max Sports inajitahidi kuwaletea habari za vijana wetu na wadau wa michezo duniani...


Tunakutakia heri Salim Juma Zongo kwenye masomo na maendeleo yako kwenye michezo na maisha kwa ujumla...

1 comment:

  1. Good job Salim.. What a way to represent Tanzania. God bless you abundantly uendelee vizuri.. Real talk..

    ReplyDelete