Tuesday 13 May 2014

CONGO PLAYOFFS: WATU 15 WAMEPOTEZA MAISHA KATIKA MECHI YA ASV NA TP MAZEMBE


Ulimwengu wa soka wa Congo uko katika majonzi baada ya watu 15 kupoteza maisha na watu 21 kujeruhiwa huko Kinshasa, Demokrasia ya Congo....Ugomvi ulianza wakati mechi inaendelea na Tout Puissant Mazembe wakiwa mbele kwa bao moja mashabiki wa pande zote mbili wakaanza fujo na kurusha vitu uwanjani wakitaka refa asimamishe mchezo...Baada ya hapo polisi walirusha mabomu ya machozi na kuwachanganya mashabiki ndipo watu wakaanza kukanyagana wakitafuta pakwenda...Hizi timu 2 ni timu maarufu sana huko Congo...ASV ni timu maarufu sana huko Kinshasa na Tout Puissant Mazembe ni timu kubwa sana na mabingwa kutoka Lubumbashi na mmiliki wake ni tajiri sana na ni gavana wa jimbo la Katanga anaitwa Moise Katumbi...Timu hizi zikikutana lazima kuwe na msuguano na polisi wanaimarishwa kila wakikutana...Wachezaji wawili wa Tanzania nao pia wamenusurika kwenye vurugu hizo...Hao ni Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu...CAF kupitia mwenyekiti Hayatou amsema wamesikitika sana na hizi habari....Bofya usome zaidi hapa...

No comments:

Post a Comment