Sunday 25 May 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE FINALS: REAL MADRID MABINGWA 2014


Real Madrid wamenyakua kombe kubwa sana la UEFA Champions League huko Lisbon, Portugal...Mabingwa hawa walichukua kombe mbele ya Zenadine Zidane ambaye alikuwa mchezaji wa Real Madrid wa zamani na kikosi chake ndicho kilichukua kombe mara ya mwisho...Mambo hayakuwa kama yalivyo tarajiwa lakini habari ndio hiyo na pia rafu zilikuwa nyingi na ngumi zilikuwa karibu zichapwe mara nyingi...Refaalijitahidi sana kuweka mambo sawa...



Atletico walikuwa makini sana kipindi cha kwanza lakini walichemsha na kumwingiza Diego Costa ambae ni majeruhi na hakukaa sana akatolewa...Lakini baada ya hapo Atletico walicheza mpira sana na kuwakabili Real...Real Madrid walianza kwa uoga na mpira wao ulikuwa sio wadau walivyowazoeakuwaona wakicheza...Mnamo dakika ya 36 Diego Godin aliwaweka Atletico mbele...Baada ya kipindi cha pili Real Madrid walianza kucheza kama kawaida yao lakini beki wa Atletico walikuwa makini sana kupangua mambo...



Kipa wa Atletico alifanya kazi kubwa sana na pia kutokana na urefu wake alipangua sana mashuti hatari kutoka kwa Ronaldo na wenzake...Mechi ilikuwa ya Atletico lakini dakika ziliongezwa nyingi na dakika ya 93 Sergio Ramos alipata bao zuri na kuwapa matumaini Real Madrid...Baada ya Bale kupachika bao lingine Atletico walisambaratika....Marcelo na Ronaldondi wakamaliza mchezo...Bofya hapa upate mambo zaidi yalivyokuwa...

No comments:

Post a Comment