Tuesday, 15 July 2014

CHESS: TANZANIA KWA MARA YA KWANZA YAPATA FIDE RANKINGS


Kwa mara ya kwanza katika historia Tanzania imepata FIDE (Shirikisho la Chess Duniani) rankings...Wachezaji 5 kutoka Tanzania wamepata ranking hizo za FIDE...Mwenyekiti wa Tanzania Chess Association, Geoffrey Mwanyika, alithibitisha haya na kuwataja waliopata rankings hizo ni pamoja na yeye Mwenyekiti (1922) Hemed Mlawa (1799) Yusuf Mdoe (1707) Mwaisumbe Emmanuel (1685) na Godlove Kimaro (1681)...


Georfrey Mwanyika (kushoto) akiwa na bingwa wa dunia Vishy Anand (katikati)

Mwanyika amesema sasa hawa wote wananafasi ya kuwa International Master na Grand Master...Sasa Tanzania kwa mara ya kwanza iko mbioni kutafuta Grand Master wa kwanza...FIDE walitangaza hizi ranking mpya baada ya michuano iliyofanyika hivi karibuni kati ya Kenya na Tanzania iliyoandaliwa na Spicenet na Kasparov Chess Foundation...Safi sana wachezaji wote wenye hizo ranking za kimataifa na Max Sports pamoja na wadau tunawatakia heri katika kutafuta Grand Master wa kwanza wa Tanzania...

No comments:

Post a Comment