Tuesday 1 July 2014

SIMBA SC: AVEVA KUIONGOZA CLUB YA SIMBA




Simba Sports Club imepata Rais mpya kabisa ambaye alikuwa mdau mkubwa wa 'Friends of Simba' Evans Aveva...Aveva alichaguliwa kwenye mkutano wa Simba uliofanyika kwa dhumuni la kuchagua viongozi wa club hiyo hapo Police Officers Mess Oysterbay...Aveva alichaguliwa kwa kura 1452 na mpinzani wake Andrew Tupa alipata kura 387...Aveva alivyo tangazwa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Damas Ndumbaro mashabiki walilipuka na kushangilia sana...Aliyekuwa makamu mwenyekiti Geoffrey 'Kaburu' Nyange sasa amekuwa makamu wa rais...Kaburu aliwashinda Kihwelo 'Julio', Swedi Nkwabi na Bundala Kabulwa...Bofya hapa upate habari zaidi...

No comments:

Post a Comment