Wednesday 9 July 2014

WORLD CUP 2014: BRAZIL YA AIBISHWA MBELE YA DUNIA

Muller akipachika la 1

Brazil jana ilipata kipigo cha mbwa ambacho hawatasahau milele kwa kuchapwa na Ujerumani 7-1 kwenye uwanja wa Estadio Mineirao...Hali ilikuwa tete kwa Brazil kwani sijui mabeki walikuwa wanakoroma au hawaoni vizuri maana wajerumani waliwafanya kitu mbaya ambayo haijawahi kutokea katika historia ya World Cup...

Kross akipachika la 3

Mechi ya jana ilianza vizuri tu lakini baada ya goli la kwanza la Muller dakika ya 11 tu mambo yakabadilika kabisa...Goli la pili liliingia dakika ya 23 kutoka kwa Miroslav Klose na ndio majanga yakaanzaia hapo...Kross akawatandika la 3 na la 4 muda huo huo yaani dakika ya 24 na 26...Dakika ya 29 Khedira akafanya mambo...Hapo ni magoli 5 ndani ya dakika 29 tu za mchezo...Ngoma haikuishia hapo baada ya mapumziko kwenye dakika ya 69 Schurrle aliwagonga cha 6 na huyo huyo akaja tena kuwaumiza dakika ya 79...

Brazil walibaki midomo wazi na macho kodo wakishangaa timu kuaibishwa hivi na wajerumani...Brazil walipata goli lakufutia tone la chozi kutoka kwa Oscar dakika ya 90...Bofya hapa upate historia ilivyo tokea...

No comments:

Post a Comment