Tuesday 29 April 2014

NBA: MMILIKI WA LA CLIPPERS NI MBAGUZI WA RANGI


LA Clippers ni timu kubwa ya NBA na msimu huu imefanya vizuri na kuingia Playoffs lakini pamoja na hayo yote inasemekana mmiliki wake, Donald Sterling, ni mbaguzi wa rangi...Hii imejitokeza hivi juzi tu baada ya kurekodiwa na kimada wake, V. Stiviano, na hizi recordings kuibuka kwenye web site moja machachari sana kwa habari moto moto za watu maarufu TMZ huko Marekani...Kwenye hizo recordings huyo mmiliki anamlalamikia kimada wake kwanini anapiga picha na watu weusi na anaziweka kwenye Instagram na anamwambia asiwalete watu weusi kwenye games za Clippers....

Mmoja wa hao watu ni mchezaji maarufu wa zamani wa LA Lakers Magic Johnson...Wadau wa mchezo huo wakesikitishwa sana na matamshi ya huyo mmiliki na pia wadhamini wa Clippers wameanza kujitoa wakati bosi mkubwa wa NBA, Adam Silver, amesema wanafanya uchunguzi na kwamba uchunguzi utaenda haraka na tutajulishwa hatma ya huyo mmiliki wa Clippers...Max Sports Blog itawaletea habari zaidi kuhusu hii habari siku zijazo... 

No comments:

Post a Comment