Wednesday 30 April 2014

CHAMPIONS LEAGUE: REAL MADRID YAIGARAGAZA BAYERN MUNICH


Real Madrid jana usiku iliigaragaza bila huruma Bayern Munich mabao 4 kwa 0...Katika hali ambayo haikutegemewa Real Madrid walikuwa wana kasi sana na uhakika wa pasi zao mpaka zikazaa matunda...Game ilikuwa na vurugu za hapa na pale pia rafu nyingi tu lakini refa ailkuwa makini sana kutuliza mambo...Bao lilipatikana kutoka kichwa kikali kilichopigwa na Sergio Ramos mnamo dakika ya 16 kutokana na set-piece...Huyo huyo Ramos alipachika la pili kutokana na set-piece nyingine iliyopigwa na Di Maria dakika ya 20...Ronaldo nae alionyesha makeke yake pamoja na kupigwa buti mara kadhaa aliipatia timu yake bao baada ya kupokea pasi nzuri ya square kutoka kwa Gareth Bale...Bao hili la Ronaldo limevunja rekodi ya mabao katika kombe la Ulaya la mabao 14 ambayo ilishikiliwa na Lionel Messi, Ruud van Nistaroy na Jose Altafini....


Haikuishia hapo Bayern waliendelea kula kichapo baada ya Ronaldo tena kufunga goli zuri la free-kick baada ya kipiga mpira chini wakati wapinzani wakiruka na hii ilikuwa dakika ya 89...Bayern wamepewa kichapo ambacho hawakutegemea mpaka wakaaza kucheza rafu zisizo na msingi...Sasa Real inasubiri mechi kati ya Chelsea na Atletico Madrid leo usiku...Bofya upate takwimu za mechi...

No comments:

Post a Comment