Monday 28 April 2014

EPL: GIGGS AIPA MWANGA WA TOCHI MANCHESTER UNITED


Hatimaye Manchester United wameweza kuona mwanga japo ni mwanga wa tochi kutoka kwa mwenzao na mchezaji bora sasa ni kocha Ryan Giggs...Manchester United ilikumbushwa na kocha wao wa muda kwamba Manchester United inaogopwa kwa vitu viwili tu...kasi na kutokata tamaa...na ndivyo walivyo fanya baada ya kuichapa timu hafifu ya Norwich City 4-0...Ushindi huu unakuja baada ya kocha David Moyes kutimuliwa baada ya kuwakosesha nafasi ya kuingia Champions League...

Kuna tetesi ambazo unazipata hapa Max Sports kwa mara ya kwanza kwamba Manchester United iko mbioni kuchukua kocha Louis van Gaal kutoka Uholanzi...Huyu kocha ni kocha ambae hana mzaa na anafundisha national team ya Uholanzi...Amewahi kufundisha timu kubwa kama Ajax, Barcelona, AZ na Bayern Munich...Pia alikuwa midfielder wa timu ya Royal Antwerp, Telstar, Sparta Rotterdam na AZ...Wakiweza kukamilisha mambo na kumchukua huyo Manchester United itarudi top 4...

No comments:

Post a Comment