Monday 28 April 2014

EPL:BASI LA YUTONG LAIOKOA CHELSEA


Wakati mwingine hatupendi kupanda mabasi lakini ukipanda wakati limepaki ni issue nyingine...Hii imetokea jana kwenye moja ya mechi kubwa sana za ligi ngumu ya Uingereza kati ya Chelsea FC na Liverpool FC katika uwanja wa Anfield....Liverpool ingeshinda ilikuwa inajihakikishia ubingwa lakini Chelsea walikuja kuwazuia...Timu zote zilianza vizuri kwa kujipanga na kufika golini kwa mwenzake lakini baada ya muda kusogea tuliona hali ikibadilika na mashambulizi yakielekezwa kwenye lango la Chelsea...

Chelsea walibadilisha tactics na mid-fielders wote wakarudi nyuma na kupaki basi la Yutong, haya mabasi utakutana nayo ukielekea Mbeya kutoka Dar na pia ukuelekea Kilimanjaro, hii iliwachanganya sana Liverpool maana walikuwa na possession muda mwingi na kila wakijaribu wanagonga tairi mara bodi...Ba wa Chelsea aliiweka Chelsea mbele kwenye dakika ya 45 dakika chache kabla ya muda wa kipindi cha kwanza kuisha baada ya uzembe wa Steve Gerrard...Williams pia aliipachika bao zuri mwishoni kabisa baada ya kupokea mpira kutoka kwa Torres...Bofya hapa upata habari zaidi kuhusu basi la Chelsea...

No comments:

Post a Comment