Thursday 10 April 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: MAN U YASHINDWA KUVUMILIA MBIO ZA MJERUMANI


Manchester United kwa mara nyingine imeaga mashindano ya Champions League kwa kunyukwa na Bayern Munich kutoka Ujerumani 3-1...Aggregate ya 4-2...Msimu wa Man u umekuwa mbovu sana na inasemekana hawataonekana kwenye Champions League kwa muda mrefu kutokana na kushuka kwa kiwango...Haya hali ya mechi ya jana ilikuwa mbio mbio tu...Bayern walikuwa wanawakimbiza Man U sana na pia Man U walikuwa wanajaribu counter attacks za hapa na pale bila mafanikio...Ila Vidic aliwasaidia sana Man U jana lakini Vidic na yeye anasepa mwisho wa msimu...


Man ndio walianza kuona lango la Mjerumani kupitia Patrice Evra kwenye dakika ya 57....Lakini muda mfupi baada ya hapo kwenye dakika ya 59 Mario Manzukic alisawazisha...Mambo hayakuwa mambo baada ya Bayern kuendelea kusakama goli la Man U mithili ya nyuki akiwa anamfukuza mwizi na ndipo Thomas Muller akawaweka Bayern mbele dakika ya 68....Badae Arjen Robben ambae alikuwa machachari sana alipachika goli zuri dakika ya 76...Man U na ndugu yao Moyez sasa inabidi wakajipange upya na itachukua labda miaka kadhaa warudi kwenye hali yao ya zamani...Kwa sasa limebaki jina tu...Bofya hapa upate habazi zaidi...

No comments:

Post a Comment