Monday 21 April 2014

BOXING: RUBIN "HURRICANE" CARTER AFARIKI DUNIA


Boxer maarufu katika dunia ya boxing Rubin "Hurricane" Carter amefariki dunia...Alifariki akiwa usingizini huko Toronto Canada kutokana na ugonjwa wa Cancer, Prostate Cancer...Carter ambae alifariki na umri wa miana 76 alikuwa boxer mkali sana miaka ya 60 na alifahamika alivyomtwanga Emile Griffith ambaye alikuwa bingwa 1963 katika round ya kwanza..."Hurrucane" alijaribu 1964 kuchukua ubingwa wa middleweight lakini alichapwa na Joey Giardello...

Rubin "Hurricane" Carter alikuwa tena kwenye habari lakini habari ambazo hazikuwa nzuri ni kwamba alisingiziwa na alipatikana na hatia ya kuua wazungu watatu kweye pub...Alienda jela 1966 mpaka 1985 wakati Jaji mmoja alipomtoa nakusema kesi yake ilikuwa imejaa chuki na ubaguzi wa rangi na hana hatia kabisa...




Toka awe huru alikuwa anapigania haki za wafungwa ambao wameonewa au wamefungwa kwa makosa ambayo sio yao...Denzel Washington mcheza filamu maarufu sana alitengeneza movie kuhusu maisha ya Rubin "Huricane" Carter insyoitwa 'The Hurricane' mwaka 1999...Soma zaidi kuhusu "Hurricane" hapa

No comments:

Post a Comment