Sunday 13 April 2014

BOXING: PAC-MAN AMCHAPA BRADLEY



Manny Pacquiao amemchapa Timothy Bradley muda si mrefu huko MGM Grand Garden Arena...Pac-Man ameshinda score cards zote za majaji na kuchuukua tena mkanda wa WBO wa welterweight...Pambano hili la marudiano lilikuwa kali lakini sio kama lililopita lakini Pac-Man alijitahidi round zote kuchapa Bradley na pia Bradley alijitahidi kurusha makonde mengi kutokana na strategy yake ya kutwanga KO Pac lakini alichemsha...Bradley hana mkono mzito wakumtoa mtu KO na alipoteza nguzu nyingi akijaribu kumtoa Pac...


Kuanzia round ya 6 Bradley alikuwa ameisha na ameumia na Pac hakupoteza muda kabisa akaendelea kumshindilia...Majaji walitoa score cards za kama hivi 118-110, 116-112 na 116-112...Wote kwa Pac...Kocha wa Pac-Man alisema bondia wake alikuwa mzembe kidogo lakini alipenda alivyo pigana na alithani Bradley anatafuta ngumi moja ashinde...Kocha wa Bradley alisema round ya kwanza ilivyoisha Tim alimwambia ameumia mguu na hakuwa na chochote cha kufaya...Bofya hapa upate mambo yalivyokuwa huko MGM Grand...


No comments:

Post a Comment