Saturday 19 April 2014

HISTORIA: KAZIDI MWAMBA; MMOJA WA WANASOKA WALIOSAHAULIKA


Kwa wale wadau wa soka wa miaka ya 60 na 70 watakumbuka kwamba miaka hiyo kulikuwa na wanasoka kutoka Afrika ambao walikuwa wazuri sana na wanafaamika duniani kote lakini dunia imewasahau kwa sababu nyingi ambazo sababu nyingine ni uzembe wa waandishi wa michezo kutowakumbuka kwa maksudi au la...Lakini hilo sasa linabadilika kupitia Max Sports na blog za michezo na websites kama hii sasa tutakuwa tunawakumbuka wachezaji wale waliokua nyota na waliosaidia soka la Afrika na michezo mingine Afrika kukua...

Mmoja wa wanasoka waliosahaulika ni Kazidi Mwamba...Kazidi Mwamba ni mwanasoka aliyetokea Jamhuri ya Demokrasia ya Congo zamani ikiitwa Zaire...Aliichezea timu ya kwanza ya waafrika weusi kuingia World Cup ya 74...Kazidi alikuwa goal keeper machachari sana miaka hiyo hata kama hawakufanya vizuri na walikuwa hawana pesa lakini kati ya wachezaji bora kutoka Afrika Kazidi ni mmoja wao...Kazidi alizaliwa March 6 mwaka 1947 huko Congo na aliichezea nchi yake katika 1968 African Cup of Nations na alikuwa mchezaji bora kwenye hayo mashindano...1974 Leopards wakashinda tena African Cup of Nations...Katika game yao ya 1974 World Cup dhidi ya Yugoslavia alifungwa magoli 3 akatolewa nje na kocha wao ambae pia alikuwa mtu kutoka Yugoslavia na kocha akamwingiza Tubilandu Ndimbi na baada ya kapo kocha alijuta kumtoa Kazidi kwani timu yao ilichapwa 9-0...

No comments:

Post a Comment