Sunday 26 June 2016

BOXING: ANTHONY JOSHUA AMLAZA BREAZEALE ROUND YA 7


Anthony Joshua amebakiza mkanda wake wa IBF baada ya kumtandika Mmarekani Dominic Breazeale ndani ya O2 Arena...Breazeale alidondoshwa round ya 7 na ni mara ya kwanza anachezea kichapo...


Joshua toka mwanzo alikuwa hatari lakini Breazeale alipokea makonde mpaka Joshua round ya 6 akaanza kukasirika...Round ya 7 Joshua alianza kurusha makonde ya kutetea kabisa na ngumi yake ya kushoto ikamshusha Breazeale chini...Sasa Joshua yuko tayari kuzichapa na watu wenye uzoefu zaidi...


Joshua amesema angependa kumuenzi Muhammad Ali kwa kuzichapa barani Africa nchini ya Nigeria au Ghana...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment