Friday 24 June 2016

FC BARCELONA: BARCELONA YACHANGIA ALISILIMIA 1.5 YA PATO LA TAIFA


FC Barcelona yachangia asilimia 1.5 katika pato la Jiji la Barcelona...Katika report iliyotolewa na kampuni ya Deloitte inasema timu ya Barcelona inachangia sana hasa katika kuajiri watu, utalii na mapato ya kodi...Mchango wa timu ya Barcelona ni Euro 906 milioni ambayo ni asilimia 1.5 ya biashara yote jijini Barcelona katika mwaka 2014-2015...


Deloitte wamesema kwa upande wa ajira tu Barcelona imetoa ajira kwa watu 16, 620...Kwa upande wa utalii asilimia 6 ya watalii wanaoingia Barcelona wanasema ni kwasababu ya timu ya Barcelona...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment