Saturday 18 June 2016

EURO 2016: ENGLAND YAWALAZA MAJIRANI


Timu ya England imefanikiwa kupata ushindi dhidi ya timu ya Wales ambao ni majirani wao katika Falme ya England huko Lens, nchini France kwa bao 2-1...


Wales kupitia mshambuliaji wake mashuhuri Gareth Bale ambaye pia anachezea timu ya Real Madrid ya Spain, aliwezesha timu yake kuongoza katika kipindi cha 1 baada ya kufunga goli la mkwaju ama free kick katika dakika ya 42... Kipindi cha pili kocha wa England Roy Hodgson alilazimika kufanya mabadiliko ambayo mchezaji Jamie Vardy and Daniel Sturridge waliingia kuongeza mashambulizi... Ilikua dakika ya 56 ambapo, Uingereza iliweza kusawazisha kupitia Jamie Vardy... 


Wales waliendelea na kazi ya kutetea goli lao ambao iliwapa England kazi ngumu hadi mpira kuingia dadika za nyongeza...Daniel Sturridge ndio akapata upenyo dakika ya 91 na sekunde ya 3 na kuifungia timu yake ya England bao la pili ambalo lilimaliza mechi hiyo kwa ushindi wa magoli mawili dhidi ya moja lililofungwa na Gareth Bale.

No comments:

Post a Comment