Tuesday 28 June 2016

EURO 2016: ITALY YAWAPELEKA SHULE SPAIN


Italy waonyesha Ulimwengu kuwa mpira hauhitaji mbwewe wa chenga nyingi ila ni ufundi wa hali ya juu sana na akili ya ziada tu...Spain ilichapwa na Italy bila ubishi tena Spain wamepata somo zuri sana na inabidi wawashukuru sana Italy...


Italy ilishinda mechi ya jana 2-0 na mabao yalitoka kwa Giorgio Chiellini dakika ya 33 na Graziano Pelle dakika ya 90+1...


Kuna gazeti moja huko Spain liliandina 'The End' au 'Mwisho' kuashiria mwisho wa Spain...Spain wameanza kupoteza dira na inabidi waanze kujipangamaana kuna vitimu vidogo lakini hatari sana siku hizi...


Kocha wa Italy ambae anahamia Chelsea, Antonio Conte, ni kocha mzuri ambae aleweza kuwachapa Belgium na Spain kwenye michuani ya Euro...Ingawa anavituko uwanjani kama Jose Mourinho lakini ni kocha makini sana...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment