Tuesday 14 June 2016

EURO 2016: GERMANY YASHINDA 2-0 DHIDI YA UKRAINE

 
Shweinsteiger

Germany imeanza vizuri michuano mikali ya Euro 2016 kwa kuwafunga Ukraine 2-1...Bao la kwanza lilitoka kwa Shkodran Mustafi dakika ya 19 na la dakika za lala salama lilitoka kwa Shweinsteiger dakika za nyonyeza mwishoni kabisa...

Mustaafi akipiga kichwa hatari kabisa...

Gumzo lilikuwa jinsi beki hatari Jerome Boateng alivyookoa bao kwenye mstari...Boateng alipiga sarakasi fulani hivi wakati anaokoa bao kwenye mstari na ilibakia kama sentimita chache sana kuingia...

Jerome boateng akiokoa bao golini...

Uzuri wa teknologia ya golini au goal-line technology ndio ilionyesha mpira haujaingia maana ingekuwa utata sana...

Toni Kroos

Pamoja na yote Germany bado hawajakaa sawa sawa...Kuna wakati unaona kabisa defense inazeembea na kipa anabaki kuokoa nafasi za Ukraine...Kifaa kilikuwa Toni Kroos katika midfield...Kroos aliweza kucontrol midfield na kusaidia safu ya mbele...Tuone huko mbelei labda watabadilika...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment