Thursday 16 June 2016

UGANDA: MABONDIA WAWILI WAGANDA WAINGIA MITINI HOLLAND



Mabondia wawili kutoka Uganda (pichani) ambao walikua  kwa mwaliko wa mazoezi na kujifua kwa ajili ya matayarisho ya Olympics wametoweka katika mazingira ya kutatanisha...Mambondia hao wawili ambao majina yao yametajwa kuwa ni Atanus Mugerwa na Sula Segawa walionekana mwisho wikiendi ambapo waliondoka bila kutoa taarifa yoyote...Wakati wakiwa Uholanzi, mabondia hao ambao ni ngazi ya Bantam na Lightweight walikua chini ya uangalizi wa bondia muholanzi anayejulikana kwa jina la Andaman Daku...Msemaji wa shirikisho la mabondia kutoka Uganda amesema "mabondia hawa walikua wazuri sana na hadi sasa hatuna maneno ya nyongeza kwani tumepoteza uwezo wa kudhibiti mazingira yalikua yanawazungua mabondia hao"

No comments:

Post a Comment