Tuesday 14 June 2016

COPA AMERICA: BRAZIL YATOLEWA NJE NA PERU


Kwa mara ya kwanza katika miaka 30 Brazil imeaga michuano ya Copa America...Brazil imetolewa na Peru kwa kuchapwa 1-0 katika makundi...Pamoja na kulalamika kuwa bao walilofungwa na Raul Ruidiaz dakika ya 75 ni la mkono lakini matokeo yanabaki palepale...Mpira ulichelewa dakika 5 wakati refa anawasiliana na marefa wenzake kabla ya kuruhusu goli...Kocha wa Brazil, Dunga, amesema haogopi kuhusu kibarua chake baada ya kutolewa mapema...Peru haijawahi kuifunga brazil toka mwaka 1985...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment