Thursday 16 June 2016

NBA FINALS: MECHI INAYOSUBIRIWA SANA NI YA IJUMAA KUANGALIA KAMA LEBRON ATAIPAISHA CAVS AU LA

 
 
Mchezaji kiungo wa mpira wa kikapu anayechezea Cleveland Cavaliers, LeBron James, ameendelea na kuonyesha umahiri wake na kuwezesha timu yake kuidhibiti timu ya Golden State Warrior baada ya kuwa na mwanzo mbaya katika finali za NBA nchini Marekani...Akisaidiwa na Kyrie Irving hao wawili wamekuwa mihimili ya Cavs mpaka sasa... 
 

Cavaliers ambayo walikua wako nyuma kwa mechi mbili wameweza kucheza vizuri na ndani ya Game 5 ambayo mechi ya mwisho ilichezwa usiku wa Jumanne na kuwawezesha kupunguza idadi ya mechi za ushindi dhidi ya Golden State hadi kufikia 3-2...


Fainali hizo ambazo huchukua mechi saba kupata mshindi zinategemea kuendelea siku ya Ijumaa tarehe 17 ya mwezi June katika kiwanja cha nyumbani cha Cleveland Cavaliers...Mechi hiyo ndio itakuwa ya kuamua ni nani atakuwa mshindi wa mashindano hayo ya NBA kwa mwana 2016...

No comments:

Post a Comment