Sunday, 31 July 2016
SIMBA SPORTS CLUB: SIMBA YAFANYA MAAMUZI YA KUBADILIKA NA KUWA KAMPUNI
Simba Sports Club wameamua kwa pamoja kubadilika na kuwa timu ya kisasa...Wamekubali kuendesha shughuli za timu kikampuni zaidi...
Dewji au kwa jina maarufu 'MO' anataka kutoa 20 billion achukue asilimia 51 ili kuiwezesha timu iendeshwe kisasa...
Mdau mashuhuri wa Max Sports na mdau mkubwa sana wa Simba SC, Octavian Mshiu, alikuwepo kushuhudia historia ambayo imewekwa na wadau wa Simba...Taswira hizi ni kwa hisani ya mdau Mshiu...Kila la heri Simba SC kwa mabadiliko haya ya kihistoria...
BOXING: CARL FRAMPTON AMCHAPA KWA POINTS SANTA CRUZ NA KUWA BINGWA WA WBA FEATHERWEIGHT
Carl Frampton amemchapa Leo Santa Cruz katika mechi kali sana iliyoishishia kwenye points jijini New York...Frampton amenyakua ubingwa wa dunia WBA featherweight kwa majaji wawili kuamua ameahinda na jaji mmoja kuamua pompano ni draw...Ni mara ya kwanza Santa Cruz anachapwa na ni mara ya kwanza Frampton anazichapa katika uzito wa featherweight baada ya kupanda uzito kutoka bantam...
Pambano lilikuwa kali sana mpaka mwisho na kama ulikosa endelea kusoma habari hapa Max Sports utapata dondoo za video ya fight...Bofya hapa upate habari zaidi.
F1: LEWIS HAMILTON AMESHINDA GERMAN GRAND PRIX
Lewis Hamilton ameshinda German Grand Prix...Hamilton alianza wa 2 kwenye grid lakini aliweza kuanza vizuri na kumpita Nico Rosberg kanla ya corner ya kwanza...Hamilton aliongoza mwanzo mwisho...
Ricciardo na Max Verstapen wa Red Bull wamechukua nafasi ya 2 na 3...Ni GP ya 100 kwa Ricciardo...Bofya hapa upate habari zaidi.
Saturday, 30 July 2016
CHICAGO CUBS: UMPIRE AMSUKUMA JAVIER BAEZ
Katika hali ya kawaida umpire (refa wa baseball) huwa hasukumi mchezaji lakini katika tukio hili infielder wa Chicago Cubs, Javier Baez, alimsukumwa na umpire alivyofika tu kwenye plate na wakati anamsaidia mchezaji mwenzake...Kisa Baez alimziba umpire na ikabidi asukumwe ili umpire alone vizuri...Bofya hapa upate habari zaidi.
F1: HAMILTON ACHUNGUZWA KUTOKANA NA KUTOKA PIT BILA UANGALIFU
Lewis Hamilton yuko chini ya uchunguzi kutokana na kutoka pit stop bila kuwa makini....Wakati anatoka team Haas nao walikuwa tayari wameweka na Hamilton anatoka mbele yao...
Kama akukutwa na hatia ataanza nafasi ya 10 mashindano ya kesho Germany...Bofya hapa upate habari zaidi.
ROGERS CUP 2016: MONFILS AMEMTOA MKALI WA CANADA RIONIC
Gael Monfils kutoka France amemchapa mkali wa tennis Canada Milos Rionic sets zote ndani jiji la Toronto...Monfils ni namba 14 ameonyesha uwezo wake kwa kumchapa namba 4 duniani Rionic 6-4 6-4...Djokovic nae alifanikiwa kumchapa Byrdych kwa shida....Bofya hapa upate habari zaidi.
Friday, 29 July 2016
F1: UZIO WA MAGARI YA F1 'HALO' KUTOTUMIKA MSIMU WA 2017
Ferrari na uongozi wa F1 walianza kutengeneza 'halo' au uzio wa magari ya F1 kuzuia magereva kuumia katika ajali lakini kuna upande wa Strategy Group ambayo inaongozwa na boss wa F1 Bernie Ecclestone wamepinga na kusogeza mbele mpango huo...Sasa mpango huo hautakuwepo msimu ujao na unaweza kuanza msimu wa 2018...
Madereva wengi wakiwemo Lewis Hamilton na Sebastian Vettel wamesema usalama wao ni muhimu zaidi na itabidi waongeze hiyo halo...Bofya hapa upate habari zaidi.
GONZALO HIGUAIN: HIGUAIN AMESEMA ATAONYESHA THAMANI YAKE YA MILIONI 75.3 POUNDS NDANI YA JUVE
Katika transfer za bei mbaya ya Gonzalo Higuain kwenda Juve kwa dau la milioni 75.3 nayo imo...Higuain amesema ataonyesha thamani yake ndani ya Juve...Gonzalo mwenye umri wa miaka 28 amesaini mkataba wa miaka 5 na Juve...Higuain alikuwa anaichezea Napoli ambapo mmiliki wa Napoli, Aurelio De Laurentiis, amemuita Higuain msaliti alivyohamia Juventus...Hao wawili hawaelewani kabisa...
Higuain alishinda Golden Boot ya Italy inayoitwa Capocannoniere kwa kumaliza ligi ya Serie A akiwa na maba 36 ambayo ni sambamba na rekodi ambayo ipo...Bofya hapa upate habari zaidi.
ARSENAL FC: MLS ALL-STARS YACHAPWA NA ARSENAL 2-1
Arsenal imeshinda mechi dhidi ya wakali wa ligi ya America MLS maba 2-1 ndani ya uwanja wa San Jose Earthquakes wenye jina la Avaya Stadium...
Joel Campbell, Costa Rican International, alianza kwa kuiweka Arsenal mbele kwa kupitia tuta...
Alipachika bao safi upande wa kushoto mwa kipa na kipa aliufwata lakini ulikuwa na kasi ya ziada...
Mkali wa Chelsea wa zamani Didier Drogba alisawazisha bao la MLS All -Stars...
Mwishoni dogo Chuba Akpom alipachika bao la ushindi akipokea cross kutoka kwa Nacho Monreal...
Granit Xhaka nae alicheza kwa mara ya kwanza kabisa toka atoke Borussia Monchengladbach...
Oxlade-Chamberlain alicheza vizuri sana na alipata 'shot on goal'...Bofya hapa upate habari zaidi.
Thursday, 28 July 2016
MANCHESTER CITY: EVERTON DEFENDER JOHN STONES ANATAFUTWA NA CITY
Beki wa Everton, John Stones, anatafutwa na Manchester City na maongezi bado yanaendelea...Everton wanataka 50 milioni pounds kumchukua dogo mwenye umri wa miaka 22...Stones alitokea Barnley na ilikuwa karibu aingie Chelsea...Stone alikuwa kwenye squad ya England ya Euro 2016 lakini hakucheza...Bofya hapa upate habari zaidi
MICHAEL SCHUMACHER TRIBUTE MATCH: MANY SPORTS PERSONALITIES CAME OUT FOR A CHARITY TO HONOR MICHAEL SCHUMACHER
A lot of sports personalities came out for a charity match to honor Formula 1 legend Michael Schumacher in Germay.
RIO OLYMPICS 2016: USAIN BOLT NDANI YA BRAZIL
Usain Bolt kaingia Brazil kwa pipa tayati kuweka historia katika Olympics za mwaka huu...Bolt anafukuzia 'triple-triple' medani 3 katika mashindano matatu tofauti...100m, 200m na sprint relay...
Olympics imekumbwa na mizengwe mingi na Bolt atasaidia kuichangamsha Olympics za Rio de Janeiro...Bofya hapa upate habari zaidi
ARSENAL FC: ARSENAL WAJIWEKA SAWA KAMBINI NDANI YA SAN JOSE TAYARI KUCHEZA NA MLS-ALLSTARS
Wenger akiwa na Xhaka |
Arsenal iko kambini ikijifua na leo usiku itapambana na MLS-Allstars...
Arsenal walitumia uwanja wa Stanford University kujifua ipasavyo...
Wakali wa huko ni Didier Drogba, Andrea Pirlo na Kaka...
Beki wa kati ambae Arsene Wenger anamuamini Calum Chambers atakuwa ndani ya sqaud ya leo...Bofya hapa upate habari zaidi.
ARSENAL FC: BEKI WA KATI FABIAN SCHAR ANASAKWA NA ARSENAL
Arsenal bado wanahitaji kujaza nafasi za mabeki na sasa wanamwinda beki wa kati Fabian Schar...Schar anatoka Switzerland na anachezea timu ya 1899 Hoffenheim...Kwa sasa Per Mertesacker atakuwa nje miezi kadhaa katokana na majeraha na Lauren Koscienly yuko likizo ya ziada...Bofya hapa upate habari zaidi.
Tuesday, 26 July 2016
FIFA WORLD CUP: AFRICA KUPEWA NAFASI 2 KAMA MASHINDANO YATAPANUKA ASEMA INFANTINO
Boss wa Fifa, Gianni Infantino, amesema Africa itapata nasafi 2 za World Cup finals kama mashindano yataongeza timu mpaka 40...Kabla hajachaguliwa kuongoza Fifa Infantino alipendekeza timu ziongezwe...Kwa sasa Africa ina nafasi 5 tu...Kama timu zitaongezwa itakuwa kuanzia mwaka 2026...Bofya hapa upate habari zaidi.
MICHAEL JORDAN: JORDAN AFUNGUKA KUHUSU MAUWAJI YA WATU WEUSI MIKONONI MWA POLICE NCHINI MAREKANI
Michael Jordan, mwanamishezo mashuhuri sana na tajiri, amefunguka na kuongea juu ya mauaji yanayoendelea nchini USA ya watu weusi mikononi mwa polisi...Amesema hawezi kukaa kimya kwa sababu anaelewa jinsi gani familia za wafiwa zinapitia nini kwani baba yake mzazi aliuwawa kwa risasi na watu waliotaka kuiba gari yake mwaka 1993...Jordan amesema mambo yanayoendelea inabidi yaache kwani America ni nzuri zaidi ya maovu...Jordan ametoa $2 milioni kwenda kwa vyama viwili ambavyo sio vya Serikali vyakusaidia watu kwenye mikasa kama hii...Bofya hapa upate habari zaidi.
ANTONIO CONTE: CARLOS TEVEZ AMTOLEA NJE CONTE
Katika harakati za kuimarisha safu ya Chelsea Antonio Conte aliamua kumfukuzia Carlos Tevez lakini Tevez ametoa nje...Safu ya mbele ya ya Diego Gosta akisaidiwa na Michy Batshuay inaonekana badi inahitaji mtu wa kuisaidia na alitaka Tevez aje lakini Tevez kachomoa...Kwa sasa Tevez anachezea Boca Juniors na amesema msimu huu hato rudi Premiership...Bofya hapa upate habari zaidi.
ROGERS CUP 2016: DOG AMSHANGAZA KYRGIOS
Bingwa wa Wimbledon kwa upande wa vijana, Denis Shapovalov, amemchapa namba 19 duniani Nick Kyrgios katika round ya kwanza ya Rogers Cup huko Toronto, Canada...Kyrgios anayetokea Australia alitandikwa 7-6 (7-2) 3-6 6-3...
Kyrgios amekubali alicheza ovyo...Ni mara ya 2 tu dogo Shapovalov mwenye umri wa miaka 17 anacheza michuano ya ATP...Atakutana na Grigor Dimitrov wa Bulgaria...Bofya hapa upate habari zaidi.
Monday, 25 July 2016
TOUR DE FRANCE 2016: FROOME ASHINDA TENA TOUR DE FRANCE
Chris Froome na timu yake ya SKY wameshinda Tour de France kwa mara ya 3 sasa...Kabla ya mwaka 2008 Froome alikuwa anaendesha biskeli na timu ya Kenya...Yeye ni mzaliwa wa Kenya lakini raia wa England...
Ni kati ya waendesha baiskeli wachache ambao wameweza kushinda Tour de France mara 3...Ni mtu wa 8 kumaliza wa 3 katika historia ya Tour de France...
Froome aliweza kuingia Paris kwa ustaa akiwa na Champagne na Beer kabla ya mbio za mwisho...Bofya hapa upate habari zaidi.
DALAS COWBOYS: BASI YA DALAS COWBOYS LAPATA AJALI WANNE WAPOTEZA MAISHA
Basi la Dallas Cowboys limepata ajali likiwa linaelekea Las Vegas...Watu wanne wamepoteza maisha baada ya basi la Dallas Cowboys kugongana na gari dogo aina ya Van na kutoka nje ya barabara...Basi hilo lilikuwa limebeba wafanyakazi wa Cowboys na hakukuwa na mchezaji hata mmoja...
Watu wote waliopoteza maisha walitoka gari dogo...Bofya hapa upate habari zaidi.
Sunday, 24 July 2016
F1: LEWIS HAMILTON AMEMPITA NICO ROSBERG KWA POINTS BAADA YA KUSHINDA HUNGARY GP
Ingawa kuna wakati gari yake ilikuwa inapunguza mwendo kutokana na matairi kuisha lakini alifanikiwa kuingia kwenye pit lane akiwa na muda wakochomoka na kumalizia shindano...
Rosberg alichukua nafasi ya 2 na Ricciardo nafasi ya 3...Bofya hapa upate habari zaidi.
IOC: WANARIADHA WA RUSSIA AMBAO WAKO SAFI KURUHUSIWA KUSHIRIKI OLYMPIC
International Olympics Committee (IOC) wamebadilisha uamuzi wao wa kufungia Russia kabisa na sasa itaruhusi wanariadha safi tu kushiriki...Wanariadha watapitia uangalizi wa ziada kabla ya kushiriki Olympics...Russia ilifungiwa kutokana na kuhusika na utumiaji wamadawa ya kuongeza nguvu...Uamuzi huu umeshangaza wengi na unaonekana kuwaonea huruma Russia...Bofya hapa upate habari zaidi.
LONDON ANNIVERSARY GAMES: BOLT AWIKA MASHINDANI YA MITA 200
Usain Bolt wa Jamaica amwika katika mashindano ya riadha ya London Anniversary Games ndani ya Uwanjawa Olympics London..Bolt ambae ni bingwa wa Olympics mara 6 alimaliza mita 200 kwa kutumia muda wa 19:89....Bolt aBofya hapa upate habari zaidi
NATIONAL RALLY CHAMPIONSHIP: GULJIT DHANI WA MOSHI YUKO TAYARI KUPAMBANA ARUSHA
Subscribe to:
Posts (Atom)