Tuesday 12 July 2016

AFRICAN CHAMPIONSHIP RALLY: RANDEEP BIRDI AWIKA RALLY YA BAGAMOYO

Randeep Birdi (kawowo sports)

Randeep Birdi amefanikiwa kushinda round ya 4 ya African Rally Championship (ARC) Rally iliyofanyika Bagamoyo...Birdi alikuwa ndani ya Mitsubishi Evo 9 akiwan na navigator Zubayr Peredina amekuwa mtanzania wa 3 baada ya Omar Bhakresa na Gerald Miller kushinda michuano ya bara (continental level rally)...

Gerald Miller 

Watanzania wamechukua nafasi zote 3 za juu huku Jamil Khan alichukua nafasi ya 2 na mkongwe Gerald Miller alichukua nafasi ya 3...Magari 12 kati ya 25 yalifanikiwa kumaiza kilometer 500 za mashindano...Wengine waliofanikiwa kumaliza 5 bora ni mkali Dharam Pandya na mkongwe kutoka Uganda Cristakis Fitidis...Wengine waliojitahidi ni Ajminder Singh kutoka Kilimanjaro ambae alichukua nafasi ya 6 akiwa ndani ya Subaru Impreza na mjukuu wa Pano Calvrias, Anastasios Calvrias, alikamata nafasi ya 7...


Kwa mashindano haya inaonekana Mitsubishi Evo ilitamba dhidi ya Subaru kwani wote waliochukua nafasi za juu walikuwa mitsubishi Evo...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment