Showing posts with label #Rio2016. Show all posts
Showing posts with label #Rio2016. Show all posts

Friday, 12 August 2016

RIO 2016: KOCHA WA KENYA ATILULIWA KWA KUTUMIA VITAMBULISHO VYA FERGUSON ROTICH


Kenya imejikuta kwenye vyombo vya habari ikiongelewa vibaya tena baada ya kocha John Anzra kurudishwa nyumbani kutokana na kujifanya yeye ni mwanariadha wa mita 800 Ferguson Rotich...Alikutwa anatumia vitambulisho vya huyo Rotich akijifanya yeye ndio Rotich...Ni shida sana kwa wanariadha wazuri wa Kenya kwani wanapewa sifa mbaya kwasababu ya wajinga wachache...Rotich yuko tayari kukimbia katika mashindano ya riadha leo...Bofya hapa upate habari zaidi.

RIO 2016: MTANZANIA HILAL HEMED HILAL AMEJITAHIDI SANA KWENYE SHINDANO LA SWIMMING


Hilal Hemed Hilal ametuwakilisha vyema kwenye mashindano ya swimming huko Rio de Jenairo kwa kushinda heat ya 4 na kuweka rekodi yake binafsi na ya nchi ya muda wa 23:70...Walikuwa washindani 8 katika heat ya 4 na Hilal akaibuka wa kwanza kabisa...Bado tuna matumaini ya kupata medani lakini kwa sasa tusubiri kidogo...Pongezi sana Hilal Hemed Hilal...Bofya haha upate kuangalia jinsi Hilal alivyoshinda heat ya 4.

Tuesday, 9 August 2016

RIO 2016: BRAZIL YASHINDA DHAHABU YA KWANZA KUPITIA MCHEZAJI WA JUDO RAFAELA SILVA


Judoka, Rafaela Silva, ameshinda medani ya dhahabu ya kwanza kwa Brazil...Rafaela Silva ametokea uswazi au kwa jina maarufu huko brazil favela mpaka kuwa bingwa wa judoka...Rafaela ametokea eneo la 'City of God' ambalo ni la watu wa chini na lina watu wengi sana na maisha magumu sana...


Kwa mara ya kwanza Olympics inafanyika South America na Brazil ni sehemu muhimu sana kwani ni nchi yenye utajiri mkubwa lakini tofauti ya maskini na tajiri ni kubwa sana...


Rafaela alifanikiwa kumtoa namba 1 duniani katika uzito wa 57kg Judo, Sumiya Dorjsuren, anayetokea Mongolia...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 28 July 2016

RIO OLYMPICS 2016: USAIN BOLT NDANI YA BRAZIL


Usain Bolt kaingia Brazil kwa pipa tayati kuweka historia katika Olympics za mwaka huu...Bolt anafukuzia 'triple-triple' medani 3 katika mashindano matatu tofauti...100m, 200m na sprint relay...


Olympics imekumbwa na mizengwe mingi na Bolt atasaidia kuichangamsha Olympics za Rio de Janeiro...Bofya hapa upate habari zaidi

Sunday, 24 July 2016

IOC: WANARIADHA WA RUSSIA AMBAO WAKO SAFI KURUHUSIWA KUSHIRIKI OLYMPIC


International Olympics Committee (IOC) wamebadilisha uamuzi wao wa kufungia Russia kabisa na sasa itaruhusi wanariadha safi tu kushiriki...Wanariadha watapitia uangalizi wa ziada kabla ya kushiriki Olympics...Russia ilifungiwa kutokana na kuhusika na utumiaji wamadawa ya kuongeza nguvu...Uamuzi huu umeshangaza wengi na unaonekana kuwaonea huruma Russia...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 22 July 2016

RIO OLYMPICS 2016: WANARIADHA WA RUSSIA WAFUNGIWA KUSHIRIKI RIO 2016



Chama cha Olympics kimewafungia timu ya  Russia kushiriki katika Rio Olympics kutokana na ripoti ambazo zimetoka zinazosema Russia imehusika kuficha maovu na kuendekeza madawa ya kuongeza nguvu...Baada ya kufungiwa Russia walijaribu sana kubadilisha uamuzi huu lakini wamegonga mwamba...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday, 19 July 2016

RIO 2016: RUSSIA WANAWEZA KUFUNGIWA KUCHEZA RIO 2016


Wakuu wa Olympics kukaa na kuamua kama Russia watahudhuruia Rio 2016...Report iliyotoka hivi karibuni imebaini Russia ilikuwa na mpango kwa miaka 4 ya kuwaongezea nguvu wanariadha wao huku wakipotezea majibu ya vipimo ambavyo hubaini kama mwanariadha anatumia madawa ya kuongeza nguvu au la...Kutokana na hiyo report shirika la kuzuia matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu (WADA) limetoa pendekezo kuwa Russia ifungiwe Rio 2016...


International Olympic Committee (IOC) itaamua kuhusu suala la Russia...Russia wameomba wasifungiwe Rio 2016... Bofya hapa upate habari zaidi.