Tuesday, 31 May 2016

SPAIN: HECTOR BELLERIN PICKED TO PLAY FOR THE SPANISH SQUAD


Hector Bellerin from Arsenal is inside the Spanish squad.

INTERNATIONAL FRIENDLIES: RATIBA YA MECHI YA LEO (GMT)

TUESDAY 31ST MAY 2016

NBA: OKLAHOMA WAPATA KIGUGUMIZI WARRIORS CHUKUA WESTERN CONFERENCE


Katika hali ambayo haikutegemewa lakini ilikuwa sahihi Golden State Warriors wamefanikiwa kuwa maingwa wa Western Conference.

BOATENG: BEKI WA TIMU YA GERMANY JEROME BOATENG ASIKITISHWA NA KAULI YA KIBAGUZI ALIYOTOA KIONGOZI WA SIASA ZA MRENGO WA KULIA


Jerome Boateng ni mjerumani ambae baba yake anatokea Ghana ni mchezaji wa timu ya taifa ya Germany na Bayern Munich kama beki amesikitika na matamshi ya kiongozi wa siasa wa mrengo wa kulia wa chama cha AfD, Frauke Petry, ambae alisema kuwa wajerumani wengi wasingependa kuwa jirani ya Boateng...Matamshi hayo ya kibaguzi yamekasirisha watu wengi mpaka Waziri Mkuu kanena...Huyo mpuuzi ameomba radhi lakini pia amesema vibaya Mesut Ozil wakati Ozil ameenda kwenye hija huko Mecca...


Mesut Ozil akiwa Haj...
Kuna tatizo kubwa la ubaguzi nchini Ujerimani lakini watu sasa wanamwamko na tabia hizi zinapigwa vita sana...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 30 May 2016

BOXING: TONY BELLEW AMCHALA ILUNGA MAKABU


Tony Bellew amchapa Ilunga Makabu anayetokea DR Congo na kuchukua mkanda uliokuwa wazi wa WBC cruiserweight ndani ya Goodison Park...Ni mara ya kwanza Goodison Park wameonyesha pambano la Boxing na watu walijitokeza kwa wingi tu kushuhudia pambano la kimataifa...


Bellew alikalishwa chini kwenye canvas na ngumi ya kushoto round ya kwanza lakini badae alimtandika Makabu na left hook hatari na badae right upper cut hatari pamoja na  makonde ya kutosha na kufanya Makabu akose fahamu na ndio ikawa mwisho wa mchezo...


Bellew amekubali Makabu amemvunja pua lakini amevumilia na kupata mkanda ambao ni muhimu...


Sasa Bellew anamtaka David Haye au Denis Lebedev...Bofya hapa upate habari zaidi. 

INDIANAPOLIS 500: ALEXANDER ROSSI ASHINDA INDY 500


Alexander Rossi ashinda Indianapolis 500...Ni shindano la 100 hapo Indianapolis kwahiyo shamrashamra zilikuwa nyingi...Rossi ameshinda shindano lake la kwanza na ni mara yake ya kwanza kushindana...


Rossi alikuwa timua ya F1 ya Marussia na sasa ni bingwa wa Indy 500 mwaka huu...Rossi ni dereva anayeendesha gari la Andretti Autosport anasema hajui jinsi walivyoshinda maana ametokea wa 11 mpaka wa 1...

Lady Gaga nae alishuhudia Indy 500. Hapa yuko na kongwe
Mario Andretti bingwa mwaka 1969 na mshindi wa
bingwa wa dunia F1 mwaka 1978

Mshindi wa 2 ni Carlos Munoz ambae pia yuko Team Andretti Autosport na wa 3 ni Joseph Newgarden...Bofya hapa upate habari zaidi.

OLYMPIAKOS: MCHEZAJI WA OLYMPIAKOS ALAN PULIDO AMETEKWA MEXICO


Alan Pilido mwenye umri wa miaka 25 ametekwa na watu wasiojulikana huko Mexico kaskazini wakati akitoka kwenye party na wenzake...Watu waliomteka walizunguka gari yake na kumchukua katika mji unaoitwa Ciudad Victoria ambako ni karibu na nyumbani kwao...Polisi wanawasaka hao watu...Dodo huyu anaichezea timu ya Olympiakos na pia amewahi kuichezea timu ya Taifa ya Mexico...Bofya hapa upate habari zaidi.

F1: LEWIS HAMILTON AMSHUKURU NICO ROSBERG


Lewis Hamilton amemshukuru dereva mwenzake wa Mercedes, Nico Roseberg, kwa kumwachia ampite kutokana na gari ya Nico kukosa nguvu huko Monaco GP...


Team Mercedes walimwambia Nico ampishe mwenzake kwakuwa gari haina nguvu na Lewis anaenda mwendo wa kasi anaweza kupambana na Ricciardo wa Team Red Bull...


Kilichomtokea Ricciardo ni bahati mbaya kwenye pit stop wakati pit crew ilijichanganya na wakachukua mataiti ambayo sio na kupoteza muda na Lewis akampita wakati anatoka pit lane...


Ni ushindi wa kwanza mwaka huu Lewis anasherehekea kwani majanga wamemkuta sana Lewis toka aanza msimu...Mara ya Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday, 29 May 2016

CHAMPIONS LEAGUE FINALS 2016: REAL MADRID MABINGWA


Real Madrid wamenyakua kombe kubwa kuliko yote la Champions League jana usiku....Real Madrid walifanikiwa kuwachapa Atletico Madrid kwenye matuta 5-3...Cristino Ronaldo ndie aliyefunga goli la mwisho kwenye tuta...Real walianza mpira kwa kushambulia sana lakini beki ya Atletico Madrid ilikuwa makini sana na waliweza kutuliza kasi ya Real...


Real ndio walioanza kufunga dakika ya 15 kupitia Sergio Ramos bao ambali lilikuwa na utata kutokana na kuwa offside na badae nyota wa Atletico Antoine Griezmann alikosa penalty...Badae dakika ya 76 sub Yannick Carrasco aliwaweka level Atletico...


Atletico Madrid wamepoteza nafasi kubwa kwani walicheza vizuri kuliko Real Madrid...Mpaka mwisho wa dakika za nyongeza walikuwa sare 1-1...


Ni mara ya 11 Real Madrid wanabeba hii kombe kubwa Ulaya...Atletico Madrid wamefika fainali mara 3 bila kuchukua kombe na ni mara nyinngi kuliko timu yoyote...


Ni ushindi wa kwanza wa kocha Zinedine Zidane ambae alikuwa mchezaji wa Real miaka ya nyuma na ni kocha wa kwanza kutoka France kushinda Champions League...Bofya hapa upate habari zaidi.

NEDBANK CUP: SUPER SPORT BEATS ORLANDO PIRATES TO LIFT THE NEDBANK TROPHY


SuperSport United have managed to stop Orlando Pirates to lift the Nedbank Cup inside the Peter Mokaba Stadium.

 

Saturday, 28 May 2016

NBA PLAYOFFS: CAVALIERS MABINGWA EASTERN CONFERENCE


King James na Cleveland Cavaliers wamechukua ubingwa wa Eastern Conference baada ya kumchapa Toronto Raptors ndani Air Canada Centre...LeBron James amaingia fainali kwa mara ya 6 mfululizo na Cavs mara ya 2....James alimaliza na points 33 rebounds 11 na assist 6...Kyrie Irving nae alisaidia sanana kuibuka na points 30 assists za kutosha kabisa....Hongereni Cavs....Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 27 May 2016

KENYA: BUNGE LA KENYA LAPITISHA SHERIA KALI ZA KUZUIA MADAWA YA KUONGEZA NGUVU KWA WANARIADHA


Bunge la Kenya limepitisha Sheria kali za kujaribu kuzuia matumizi ya madawa ya kuongeza nguzu ili kunusuru kufungiwa Olympics za  Rio 2016...Pamoja na kubadilisha Sheria bado kwa kiwango cha kimataifa hakijafikiwa wasema Wada, chama cha kuzuia madawa ya kuongeza nguvu duniani...Kenya wana wanariadha mashuhuri na wengi ambao wanaweza kuleta medani ya dhahabu kama walivyo fanya mwaka 2015 katika World Athletics Championship huko Beijing China...Sheria mpya inabidi ipitishwe na Senate halafu Rais Uhuru Kenyetta aweke saini iweze kutumika...Bofya hapa upate habari zaidi.

BAFANA BAFANA: KOCHA TED DUMITRU AFARIKI DUNIA


Ted Dumitru amefariki dunia akiwa Eastgate shopping center...Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya South Africa Bafana Bafana na kocha mwenye mafanikio kuliko wote South Africa...Mara ya mwisho kabla ya kustaafu alikuwa mkurugenzi wa ufundi timu ya Premier League ya South Africa ya Mamelodi Sundowns...Alikuwa na miaka 76...Alianza kufundisha timu za South Africa mwaka 1985 akiwa na Kaizer Chiefs...Ameshinda vikombe vingi sana na Kaizer Chiefs na pia kuchukua kombe la Premiership mfululizo...Kwa jina maarufu la "The Prefessor" amesaidia Mamelodi Sundows kushinda ligi maya 2 na kuwapeleka CAF Champions League mpaka wakawa wa 2 mwaka 2011...Pumzika kwa amani kocha Dumitru...Bofya hapa upate habari zaidi

Thursday, 26 May 2016

FRENCH OPEN 2016: RAFA NADAL ASHINDA GRAND SLAM YA 200


Mkali wa Clay Court Rafa Nadal ameshinda mechi yake kubwa ya 200 baada ya kuchapa Fancundo Bagnis 6-3 6-0 6-3 kwenye michuano ya French Open inayoendelea...Nadal anatafuta taji lake la 10 la Roland Gaross ataingia round ya 3 na Marcel Granollers...Bofya hapa upate habari zaidi.

BREAKING NEWS: JOSE MOURINHO AMESAINI MKATABA NA MANCHESTER UNITED


Habari zilizoingia Max Sports kutoka kwa wadau Uingereza ni kwamba Jose tayari amesaini mkataba mpya na Manchester United...Mazungumzo yalikuwa marefu lakini sasa wameshakubaliana na hatimaye ni kocha mpya Manchester United...


Mourinho ni kati ya makocha wenye rekodi nzuri duniani na sasa yuko tayari kuinyayua Manchester United...Dakika kama 20 zilizopita ameonekana akiwa ndani ya suti na kashikilia makabrasha na sasa tunasubiri club ya Manchester itoe rasmi tamko...

MANCHESTER UNITED: CHELSEA YASHIKILIA HATI MILIKI YA JOSE MOURINHO MAZUNGUMZO YANAENDELEA


Kocha Jose Mourinho bado hajatangazwa rasmi kuwa kocha wa Manchester United kutokana na mazungumzo yanayoendelea baina ya boss wa Manchester Ed Woodward na agent wa Mourinho pamoja na wanasheria...Chelsea wana hati miliki ambayo waliinunua mwaka 2005 na wana haki ya kutumia jina la Jose Mourinho kwenye vitu vingi na Manchester hawawezi kutumia jina hilo bila upata ruhusa kutoka Chelsea...Hati miliki hiyo inamalizika tarehe 31 March mwaka 2015...Labda ikifikia leo jiomi Mourinho atakuwa amesaini mkataba na Manchester City...Bofya hapa upate habari zaidi.

ARSENAL: STAN KROENKE AONGEZA HISA ZA UMILIKI ARSENAL


Stan Kroenke mmiliki mwenye hisa nyingi toka mwaka 2011 ameongeza hisa zake na kufikia asilimia 67.05...Kroenke pia anamiliki timu ya NFL ya Los Angeles Rams huko Marekano...Bofya hapa upate habari zaidi.

ZLATAN IBRAHIMOVIC: "NIMEAMUA TIMU GANI NITAHAMIA"


Zlatan Ibrahimovich amesema ameamua timu gani atahamia lakini hajaitaja....Striker anayetokea Sweden amemaliza mkataba wake na Paris Saint-Germain na amepata offer nyingi kutoka timu mbalimbali duniani lakini wadau wanahisi ataingia Manchester United...


Ibrahimovic amewahi kufanya kazi na Jose Mourinho wakati wakiwa ligi ya Serie A timu ya Inter Milan...Inter walishinda ubingwa wakati huo...


Ibrahimovic alianza kuichezea timu ya nyumbani kwake ya Malmo mwaka 1999 na badae akahamia Ajax, Juventus, Inter Milan, Barcelona, AC Milan na PSG...Kwa ujumla anamabao 392 katika mechi 667 na mwakajana alifanya kweli kwa kufunga mabao 50 kati ya mechi 51...Bofya hapa upate habari zaidi.

FORMULA E: PATA TASWIRA YA MASHIDANO YA FORMULA E YA MAGARI YASIOTUMIA MAFUTA


Wiki hii Formula E wako Berlin na baada ya hapo watamalizia jijini London mwezi ujao...


Formula E ni magari kama ya Formula One lakini hayatumii mafuta bali yanatumia umeme wa battery na hizo battery zinapoozwa na barafu kavu au dry ice...


Pata taswira ha mambo yalivyo huko Berlin Germany...Bofya hapa upate habari zaidi.

Alain Prost wa Renault  akipiga story a wenzake

Dry ice ikiwenkwa ili kupooza battery 

Mashabiki na wapenzi wa Formula E wakiangalia kwa makini...

Wapenzi wa Formual E kifamilia zaidi...

Bruno Senna akipiga selfie na mashabiki...

DJ wa musiki nae alikuwepo kutumbuiza mashabiki...