Friday 20 May 2016

TONY XIA: MMILIKI MPYA WA ASTON VILLA TONY XIA AMESEMA ANATAKA VILLA IWE KATI YA TIMU 3 BORA


Tajiri mpya wa Aston Villa, Dr. Tony Xia, amesema anataka kuibadilisha timu yake ya Aston Villa...Aston Villa ilifanya vibaya sana katika historia ya miaka 142 ya club hiyo na ikashika daraja kutoka Premiership kwenda Championship...Mmiliki mpya anayetokea China ni millionaire mwenye umri wa miaka 39 alitambulishwa Jumatano na sasa yuko tayari kwenda kazini...Xia ameweka £50 milioni za awali na anaongea na Roberto Di Matteo na Nigel Pearson kubadilisha mambo pale Villa Park...



Xia amezaliwa China katika mji wa Quzou nje kidogo ya Shanghai...Aliondoka nyumbani akiwa mdogo miaka 14 na kuingia Chuo Kikuu cha Beijing na alipofika miaka 19 alienda Marekani kwa miaka 6 kusokuma katika Chuo cha Harvard na Massachusetts Institute of Technology...Aliwahi kukaa Uingereza miezi 5 akiwa Chuo cha Oxford mwaka 2002 ndipo mapenzi yake na Aston Villa yalipoanza toka aende kucheki game ndani ya Villa Park... Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment