Sunday 29 May 2016

CHAMPIONS LEAGUE FINALS 2016: REAL MADRID MABINGWA


Real Madrid wamenyakua kombe kubwa kuliko yote la Champions League jana usiku....Real Madrid walifanikiwa kuwachapa Atletico Madrid kwenye matuta 5-3...Cristino Ronaldo ndie aliyefunga goli la mwisho kwenye tuta...Real walianza mpira kwa kushambulia sana lakini beki ya Atletico Madrid ilikuwa makini sana na waliweza kutuliza kasi ya Real...


Real ndio walioanza kufunga dakika ya 15 kupitia Sergio Ramos bao ambali lilikuwa na utata kutokana na kuwa offside na badae nyota wa Atletico Antoine Griezmann alikosa penalty...Badae dakika ya 76 sub Yannick Carrasco aliwaweka level Atletico...


Atletico Madrid wamepoteza nafasi kubwa kwani walicheza vizuri kuliko Real Madrid...Mpaka mwisho wa dakika za nyongeza walikuwa sare 1-1...


Ni mara ya 11 Real Madrid wanabeba hii kombe kubwa Ulaya...Atletico Madrid wamefika fainali mara 3 bila kuchukua kombe na ni mara nyinngi kuliko timu yoyote...


Ni ushindi wa kwanza wa kocha Zinedine Zidane ambae alikuwa mchezaji wa Real miaka ya nyuma na ni kocha wa kwanza kutoka France kushinda Champions League...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment