Wednesday 4 May 2016

CHAMPIONS LEAGUE 2016: ATLETICO MADRID NDANI YA FAINALI



Mechi ngumu ya nusu fainali ilikuwa kati ya Bayern Munich na Atletico Madrid...


Madrid waliingia Allianz Arena wakiwa na advantage ya goli 1 na haikuwa rahisi.

Wajerumani walitolewa nje kwa bao la ugenini kupitia Antoine Griezmann.

Xabi Alonso ndio aliwapa wajerumani mwanga lakini Griezmann akasawazisha.

Pande zote mbili zilikosa penalty muhimu sana....



Jan Oblak kipa wa Atletico alipangua penalty ya Tomas Muller.

Torres nae alikosa penalty lakini Atletico walifanikiwa kuwakabili Bayern mpaka mwisho kabisa.

Lewandowsky alifanikiwa kupata bao dakika ya 74 lakini bao hilo halikutosha na sasa Atletico wanasubiri fainali katika yao na Manchester City au Real Madrid...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment