Monday 30 May 2016

BOXING: TONY BELLEW AMCHALA ILUNGA MAKABU


Tony Bellew amchapa Ilunga Makabu anayetokea DR Congo na kuchukua mkanda uliokuwa wazi wa WBC cruiserweight ndani ya Goodison Park...Ni mara ya kwanza Goodison Park wameonyesha pambano la Boxing na watu walijitokeza kwa wingi tu kushuhudia pambano la kimataifa...


Bellew alikalishwa chini kwenye canvas na ngumi ya kushoto round ya kwanza lakini badae alimtandika Makabu na left hook hatari na badae right upper cut hatari pamoja na  makonde ya kutosha na kufanya Makabu akose fahamu na ndio ikawa mwisho wa mchezo...


Bellew amekubali Makabu amemvunja pua lakini amevumilia na kupata mkanda ambao ni muhimu...


Sasa Bellew anamtaka David Haye au Denis Lebedev...Bofya hapa upate habari zaidi. 

No comments:

Post a Comment