Sunday 8 May 2016

BOXING: SAUL 'CANELO' ALVAREZ AMTANDIKA AMIR KHAN KNOCKOUT ROUND YA 6


Mbwembwe za Amir Khan ziliishia round ya 6 wakati ngumi 1 tu hatari sana ya kulia ya Canelo Alvarez ilivyomkuta Khan kidevuni na chali akaanguka chini hoi...Khan alianza vizuri akirusha ngumi ambazo zilifika lakini kwa kuwa Canelo anakudevu kigumu hazikumshtua sana.




Khan aliongoza round 4 za mwanzo kutokana na kuwa mwepesi kurusha ngumi...Lakini alipokutana na ngumi nzito ya Alvarez round ya 6 akianguka chini bila ubishi na kulala hapo muda mrefu habari ikawa ndio hiyo...Khan hakuweza kwenda kukutana na waandishi wa habari alikimbizwa hospitali kwa uchunguzi zaidi...Badae aliweza kutweet kuwa yuko poa na kuwa ndio matokeo ya ndondi...


Baada ya kumtandika Khan sasa Canelo anamtaka Gennady Golovkin na kocha wa Alvarez baada ya pambano alienda kwenye kamba za ring na kumkaribisha Golovkin aje ndani ya ring...


Kwa sasa kwenye ulimwengu wa ngumi baada ya Floyd Mayweather na Manny Paquiao kustaafu Canelo na Golovkin ndio mwanga wa boxing...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment