Thursday 19 May 2016

EUROPA LEAGUE FINALS: SEVILLA MABINGWA TENA


Sevilla wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Europa League kwa kuwatandika Liverpool 3-1 jana usiku huko Basel...Liverpool walianza kucheza vizuri na hatimaye kabla ya mapumziko walipata bao safi kabisa kupitia Daniel Sturridge...Sturridge ni mchezaji wa kwanza kufunga bao Europa League/UEFA Cup toka Robbie Fowler afungee mwaka 2001...


Kipindi cha 2 Sevilla sijui waliambiwa nini na kocha maana walibadilisha game na kucheza kwa akili nyingi...Liverpool wakaanza kuchanganyikiwa na badae Klopp akamtoa Lallana lakini haikusaidia kwani Sevilla walikuwa wanacheza vizuri zaidi...


Katika mipira 4 iliyolenga goli mipira 3 ya Sevilla imeingia nyavuni...Wafungani wa Sevilla walikuwa Kevin Gameiro dakika ya 46 na Andujar Moreno mabao 2 dakika ya 64 na 70...


Sevilla wamefunga Sevilla wanachukua kombe kwa mara ya 3 mfululizo sasa...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment